Pages

Wednesday 30 January 2019

Prof. Ndalichako awataka wakandarasi kuongeza kasi ya ujenzi wa vyuo


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amehitimisha ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa vyuo vya elimu na mafunzo ya ufundi stadi Kanda ya Ziwa huku akiwataka wakandarasi kutekeleza wajibu wao kwa juhudi na uadilifu ili kuhakikisha wanakamilisha ujenzi kwa wakati kulingana na mikataba ya miradi husika.

Katika ziara yake Kanda ya Ziwa tangu tarehe 24 hadi 26 Januari 2019, Profesa Ndalichako alitembelea miradi mitatu ya ujenzi wa vyuo vya elimu na mafunzo ya ufundi stadi vikiwemo Chuo cha VETA cha Mkoa wa Geita, Chuo cha VETA cha Wilaya ya Chato, Chuo cha VETA cha Bukoba kwa ajili ya Mkoa wa Kagera pamoja na mradi wa ukarabati wa Chuo cha Ufundi Stadi Karagwe kinachomilikiwa na Halmashauri ya wilaya ya Karagwe.  

Prof. Ndalichako alifurahishwa na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa Chuo cha VETA cha wilaya ya Chato unaofanywa na kampuni ya CF Builders na kusema kuwa ni vyema wakandarasi wanaoonesha juhudi na uadilifu katika kazi zao wakaendelea kupewa kazi katika miradi mingine inayojitokeza badala ya kuchukua wengine ambao utendaji kazi wao hauna uhakika. 

“Nimpongeze sana huyu mkandarasi CF Builders ambaye pia ndiye aliyejenga chuo cha ufundi stadi Namtumbo ambako kwa kweli nako pia alifanya kazi nzuri na akamaliza kwa wakati. Niseme kwamba, watu wa manunuzi wawe na uzalendo. Mtu anayefanya kazi nzuri kama huyu kama anafanya kazi nzuri kwa nini hata kama kuna site (eneo au mradi) nyingine wasimpe?” alisema na kuhoji.

Alisema kuwa wakati kwa mujibu wa mkataba mradi huo unatakiwa kukamilika mwezi Agosti mwaka huu, hadi siku ya tarehe 24 Januari mwaka huu mkandarasi alikuwa mbele kwa asilimia 3.6 na kwamba matarajio yake ni kukamilisha na kukabidhi mradi ifikapo Julai mwaka huu. 

Mwakilishi wa Mkandarasi wa CF Builders, Fred Chacha alisema kuwa kampuni yao pia ilijenga na kukamilisha vyema vyuo vya VETA Singida, VETA Mara na VETA Namtumbo na ilipata ushirikiano mzuri wa VETA na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Kwa kuthamini ushirikiano huo na kutokana na ombi la Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dkt, Pancras Bujulu, CF Builders imeahidi kutoa msaada wa ujenzi wa jengo moja kwa ajili ya kituo cha huduma ya kwanza ndani ya chuo cha VETA Chato.  

Aidha, Prof. Ndalichako alionesha imani na mwenendo wa mradi wa ukarabati wa Chuo cha Ufundi Stadi Karagwe unaofanywa na Wakala wa Ujenzi Tanzania (TBA) na kuwa na matumaini kuwa nao utakamilika kwa wakati.

Hata hivyo, Waziri Prof. Ndalichako alishuhudia kusuasusa kwa maendeleo ya mradi wa ujenzi wa chuo cha VETA cha Mkoa wa Geita unaofanywa na kampuni ya Skywards Construction na kumtaka mkandarasi kuongeza kasi ya utendaji ili kufanikiwa kukamilisha ujenzi mwezi Agosti mwaka huu kulingana na makubaliano yaliyopo kwenye mkataba. 

Alisema kuwa upatikanaji wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi unapaswa kupewa kipaumbele cha hali ya juu kwani ni nguzo muhimu katika kusaidia maendeleo ya viwanda ambao ndio mwelekeo wa serikali ya awamu ya tano na ndio maana yeyote anayekwamisha juhudi za kupanua fursa za mafunzo hayo kupitia ujenzi na upanuzi wa vyuo hapaswi kuvumiliwa. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Dkt Pancras Bujulu alisisitiza kauli ya Waziri juu ya umakini katika taratibu za zabuni na manunuzi ili kupata wakandarasi sahihi wenye kufanya kazi kwa umakini na uadilifu.

Aliwaomba wakandarasi wengine pia kujituma na kuthamini na kuzingatia umuhimu wa kusimamia vyema miradi yao ili iweze kukamilika kwa ufanisi.

Katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, VETA inasimamia Ujenzi wa Chuo cha VETA cha Mkoa wa Geita wenye thamani ya Sh. 9.9 na fedha zinazogharamia mradi huo zinatokana na mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB); ujenzi wa Chuo cha VETA cha Wilaya ya Chato wenye thamani ya Sh. bilioni 10.7 ambazo ni fedha za ndani; ujenzi wa chuo cha VETA cha Mkoa wa Kagera wenye thamani ya Sh. bilioni 20 ambao unagharamiwa na Serikali ya China na ukarabati wa Chuo cha Ufundi Stadi Karagwe wenye thamani ya Sh. bilioni 4.6 fedha za ndani.


Government completes prerequisite setups for construction of VETA Bukoba




The government of Tanzania has accomplished setups of essential infrastructural requirements for commencement of the China government funded 20-billion shillings project for construction of Bukoba Regional Vocational Training and Service Centre (VETA Bukoba), the regional vocational training centre for Kagera.

Tanzania government was required to do some groundwork including improvement of the road towards the site, building structures for electricity and water and ensuring connection of the same to the site before the China government engages a contractor for construction of the planned vocational training centre. 

The Minister for Education, Science and Technology Prof. Joyce Ndalichako declared accomplishment of the task on Saturday, 26 January 2019 when she inspected the site at Burugo area during which she also inaugurated the mini and temporary water source constructed by Bukoba district authorities in collaboration with the Vocational Education and Training Authority (VETA).

Speaking after inauguration of the water source, Prof. Ndalichako said that the government has done its part and now hopes for quick procurement of contractor and thereafter construction to start soon as the people of Kagera have been eagerly waiting to see the training centre completed. 

 “I believe the procurement of the constructor will be accomplished immediately so that the construction starts. The Kagera people have been waiting for their regional VETA centre for a long time. The road was poor, we have improved it, there was no electricity now we have connected, there was no water but today I have launched this water source meant for construction activities. That means all of the tasks which the government was supposed to do before commencement of the construction work have been accomplished,” she said.

She expressed appreciation for the efforts done by VETA and Bukoba district officials to facilitate construction of the road, structures for power connection and for tapping water from the natural source.
Also she thanked people residing around the site for the cooperation which they have shown during construction of those initial structures and asked them to continue with the same spirit as the project is for their benefits