CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Thursday 28 July 2022

Madereva Bodaboda na Bajaji wahamasishwa kupata mafunzo kwenye vyuo vya VETA

 

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imewahamasisha madereva bodaboda na Bajaji nchini kupata mafunzo ya udereva kwenye vyuo vya VETA nchini ili kukidhi vigezo vya kupata leseni za kuendesha vyombo hivyo.


Hamasa hiyo imetolewa  Julai 24, 2022  jijini Dodoma wakati wa Kongamano la Kuimarisha Ushiriki wa Waendesha Bodaboda na Bajaji katika Sensa ya Watu na Makazi Agosti 2022 ambapo VETA ilialikwa kufanya maonesho.

Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Kati, Ndugu John Mwanja, aliiwakilisha VETA kwenye kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Anthony Mtaka.

Kongamano hilo limejumuisha waendesha bodaboda na Bajaji zaidi ya 3000 kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.




No comments:

Post a Comment