CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Thursday 22 February 2018

VETA Shinyanga yaanzisha kozi ya ufundi wa mitambo mikubwa



Chuo cha ufundi stadi VETA Mkoani Shinyanga, kimezindua mafunzo mapya ya ufundi wa Mitambo Mikubwa (Heavy Duty Equipment Mechanics), mafunzo ambayo yatasaidia vijana wengi kupata ajira kwa urahisi ndani ya Migodi na katika shughuli za ujenzi wa barabara.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kozi hiyo tarehe 19 Februari 2018 kwenye chuo cha VETA Shinyanga, Kaimu  Mkurugenzi wa Soko la Ajira, Mipango na Maendeleo wa VETA, Hildegardis Bitegera alisema kuwa kozi hiyo imeanzishwa  baada ya utafiti wa soko la ajira kubaini uhitaji mkubwa wa mafunzo ya ufundi stadi kwa ajili ya kusaidia sekta ya madini katika mikoa ya kanda ya ziwa.  
 
Alisema, katika hatua ya awali baada ya utafiti VETA Shinyanga ilianzisha kozi ya Ukataji na Ung’arishaji vito (Gemstone cutting Carving and Polishing) na kufatiwa na kozi ya Uendeshaji wa Mitambo Mikubwa (Plant Operations) na hatimaye kozi ya Ufundi wa Mitambo Mikubwa kwa ufadhili wa Serikali ya Canada chini ya Shirika la CICan kupitia mradi wa Uimarishaji Mafunzo kwa ajili ya Ajira (ISTEP).

“Leo tunawaambia watu, hasa vijana kuwa tuna kozi mpya yenye fursa kubwa ya ajira na kwa hivyo waje wajifunze. Kwa upande mwingine, tunawaambia waajiri, hasa katika upande wa shughuli za uziduzi (extractive) na ujenzi kuwa watarajie kutoka kwetu nguvukazi yenye ujuzi na mahiri kwenye ufundi wa mitambo mikubwa,” alisema.

Aliongeza kuwa, VETA inatarajia vilevile kuongeza kozi za Uchimbaji, Ulipuaji,na nyingine zinazohusiana na sekta ya madini.
Naye Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga Afridon Mkhomoi, alisema kuwa uanzishwaji wa kozi hiyo umewezekana kwa ushirikiano mzuri wa vyuo marafiki katika utekelezaji wa mradi wa ISTEP ambavyo ni Chuo cha New Caledonia na Chuo cha the Rockies vya nchini Canada.

Alisema, pamoja na mafunzo mengine ya uwezeshaji kwa Menejimenti, Walimu na Wafanyakazi wengine, vyuo marafiki walitoa mitambo na vifaa vingine vya kufundishia kwa ajili ya kozi hiyo.

Aliishukuru Serikali ya Canada na chuo cha College of New Colidonia (CNC) kwa ufadhili walioutoa wa vifaa hivyo vya kujifunzia kutengenezea mitambo ambavyo vimewezesha mafunzo kuanza mara moja.

Alisema, msaada huo ulichangia katika kuanzisha kozi kwa kudahili wanafunzi 20,  ambao kati yao 16 ni wa kiume na wanne ni wa kike.


“Natoa wito kwa vijana mkoani Shinyanga kuichangamkia kozi hii mpya ambayo itawapatia ajira kwa urahisi ndani ya migodi kwa kutengeneza mitambo ambayo itakuwa ikiharibika sababu wataalamu wake ni wachache,” alisema.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Thomas Katebalirwe, matarajio ya Serikali ni kupata watalamu wengi wa ufundi wa mitambo hapa nchini.

Aliwaomba VETA kuendesha kwa ufanisi mkubwa kozi hiyo akiamini kuwa baada ya miaka michache chuo cha VETA Shinyanga kitakuwa chuo cha mfano kwa mafunzo yanayohusiana na shughuli za uchimbaji na uchakataji madini.

Aidha mwakilishi  kutoka Chuo cha New Colidonia (CNC), Romana Pasca, alisema wameamua kufadhili vifaa kwa ajili ya mafunzo ili Tanzania ipate kuongeza idadi kubwa ya wataalamu wa kutengeneza mitambo kutoka ndani ya nchi, pamoja na kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.

Nao baadhi ya wanafunzi wanaosoma mafunzo hayo mapya akiwamo Calvin Msafiri, waliipongeza Serikali kwa kushirikiana na nchi ya Canada kuanzisha kozi hiyo mpya ambayo wana matumaini kuwa itawapatia ajira kwa urahisi na kuinua uchumi wa maisha yao.

Mkuu wa chuo cha VETA mkoani Shinyanga Afridoni Mkhomoi akisoma taarifa ya chuo hicho juu ya  Kozi mpya ya Ufundi wa Mitambo Mikubwa.

Kaimu Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo ya  Ufundi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Thomas Katebalirwe, akizungumza kwenye uzinduzi wa kozi mpya ya Ufundi wa Mitambo Mikubwa (Heavy Duty Equipment Mechanics) na kusema kuwa serikali inatarajia matokeo makubwa ya kupata wataalamu wake wengi wa ndani ya nchi wa kutengeneza mitambo hiyo mikubwa.

Mwakilishi wa Chuo cha New Colidonia Romana Pasca, akizungumza kwenye uzinduzi wa kozi mpya ya Ufundi wa Mitambo Mikubwa (Heavy Duty Equipment Mechanics). Kushoto kwake ni mwakilishi mwenzake kutoka chuo hichohicho, Craig Hull.




Baadhi ya vifaa ambavyo vijana watakuwa wakijifunzia kutengeneza mitambo mikubwa katika mafunzo hayo mapya.
 

18 comments:

  1. Mm naitwa samwel msuya niko dar es salaam nilikuwa naomba kuuliza kozi kwa kipindi hichi zinaanza lini za planting oparetor tafadhali naomba mawasiliano ya simu ya mkononi zangu ni 0679202500

    ReplyDelete
  2. Naitwa Edwin Philip nahitaji kujiunga na chuo nipo mwanza naweza jua Ada ya

    ReplyDelete
  3. Naitwa Edwin Philip nahitaji kujiunga na chuo nipo mwanza naweza jua Ada ya Sh ngapi na kukaa boding

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hey mwenye namba za mawasioiano za chuoni naomba anisaidie maana nawish kujoin ila before nataka kuongea nao plz mwenye nazo

      Delete
  4. Naitwa Monica makali nahitaji mafunzo ya excaveter je ada ni sh ngapi nania mda gani?

    ReplyDelete
  5. Naitwa Monica makali naitaji chuo cha mafumzo ya excaveter cha shinyanga je mafunzo yanaanza lini? Na ada sh ngapi? Na niyamda gani? Na ninaomba nisaidiwe contact no ya hapo chuoni mi niko Dodoma no yangu 0685510863

    ReplyDelete
  6. Enter your comment...nahitaji kujua kuhusu website yenu na cozi ya driving 2019 mwez wa 11 kama inapatikana namba yangu ni 0766021779

    ReplyDelete
  7. Mwenye namba za mawasiliano chuoni shinyanga naombeni jaman

    ReplyDelete
  8. Nahitaj kujua jinsi ya kujaza form zenu no 0765058930

    ReplyDelete
  9. jamani mm naitwa kombo omary naombeni mnisaidie namba ya hapo chuoni namba yangu ni 0710062637

    ReplyDelete
  10. Naomba jaman njiunge namb yangu 0629579825

    ReplyDelete
  11. mimi ni james kilingo nataka nijue ada ya ufundi mitambo shot cose na inakua kwa muda gan shot cose

    ReplyDelete
  12. Naitwa rehema maulidi naomba kujua Kam Kuna nafas ili niwez kujiunga na hii cozi nahitaj long course na ada ni Bei gani kwa kukaa boarding

    ReplyDelete
  13. Kwa majina rehema maulidi naomba nafasi ya kusom hii coz mpya katika chuo chenu naomben Kam Kuna nafas naomb kujua pia ada kwa wale wa boarding namb ni 0747542351

    ReplyDelete