CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Thursday, 22 December 2016

SHINDANO LA UBUNIFU WA UFUNDI STADI

Wewe ni kijana mwenye ujuzi wa ufundi stadi?

Je, una uwezo wa kuonesha umahiri na ubunifu wa kipekee katika ujuzi wako?
Kama ndivyo: Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) inakukaribisha kushiriki katika shindano la Ujuzi na Ubunifu katika ufundi stadi. Madhumuni ya shindano hili ni kuonesha umahiri na ubunifu wa vijana katika fani mbalimbali za ufundi stadi, hivyo kutoa taswira ya umuhimu wa ufundi stadi katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Maeneo ya kushindania
1. Ubunifu wa bidhaa: Eneo hili litahusisha uwezo na umahiri katika fani husika kwa kuonesha ubunifu katika kutengeneza na kusanifu bidhaa kwa ubora na ustadi unaoendana na kushughulikia changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii;
2. Ubunifu wa miradi: Eneo hili litahusisha ustadi katika kubuni miradi inayomwezesha kijana kujiajiri na ikiwezekana kuajiri wengine kupitia ujuzi wa fani aliyojifunza;
3. Umahiri katika fani: Eneo hili litahusisha vijana kuonesha uelewa wa fani kwa upana wake na namna wanavyoweza kutumia ujuzi walioupata kuongeza tija baada ya kuajiriwa au kujiajiri.
Vigezo vya kushiriki
1. Umri: Mshiriki anatakiwa kuwa kijana, mwenye umri kati ya miaka 15 hadi 35;
2. Uraia: Mshiriki anatakiwa kuwa Mtanzania;
3. Elimu: Ajue kusoma na kuandika Kiswahili au Kiingereza kwa ufasaha;
4. Ujuzi: awe na ujuzi wa ufundi stadi, iwe kwa kupitia mafunzo chuoni, sehemu ya kazi au namna nyingine yoyote ile;
Masharti na taratibu za Uwasilishaji
1. Idadi: Mshiriki mmoja anaruhusiwa kuwasilisha ubunifu zaidi ya mmoja lakini usizidi aina tatu;
2. Ushirikiano: Washiriki wawili au zaidi wanaweza kushirikiana kubuni na kuwasilisha ubunifu wao kama kikundi;
3. Umiliki: Ubunifu unatakiwa uwe umeandaliwa na mhusika au wahusika wenyewe. Hairuhusiwi kuwasilisha kitu au mradi ulioandaliwa na mtu mwingine;
4. Muda: Muda wa kuwasilisha ubunifu ni kati ya Novemba 25, 2016 hadi January 15, 2017;
5. Namna ya kuwasilisha: katika hatua ya awali mshiriki au washiriki wanapaswa kuwasilisha taarifa za ubunifu zikiwa na maelezo kuhusu ubunifu husika na manufaa yake katika jamii picha na/au michoro kwa ajili ya tathmini ya awali kabla ya mchakato wa mchujo.
6. Mahali pa kuwasilisha: Taarifa za ubunifu zifungwe vyema kwenye bahasha na juu yake ziandikwe “SHINDANO LA UBUNIFU”, kisha ziwasilishwe kupitia anuani:
VETA Makao Makuu,
S.L.P. 2849
Dar es Salaam
Taarifa hizo zinaweza pia kuwasilishwa kupitia barua pepe pr@veta.go.tz

7. Mchujo: Kamati maalum ya watalaam itafanya tathmini ya ubunifu na kuchagua washindi 15 bora (watano katika kila eneo la ushindani). Washindi hao 15 bora wataalikwa kushiriki kwenye maonesho ya ubunifu yatakayoandaliwa sambamba na tamasha la ajira litakalofanyika mwezi Februari, 2017;
8. Kilele cha Mashindano na Tuzo: wakati wa maonesho, kamati ya wataalam itaendelea kufanya tathmini ya ubunifu, kisha kuchagua washindi watatu bora kwenye kila eneo ambao watapewa tuzo mbalimbali:
Mshindi wa Kwanza: Shilingi Milioni Moja (1Mil.), Ngao na Cheti
Mshindi wa Pili: Shilingi Laki Nane (800,000) na Cheti
Mshindi wa Tatu: Shilingi Laki Tano (500,000) na Cheti
Kumbuka: Vijana wa kike wanahamasishwa kushiriki kwa wingi
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
Kitengo cha Uhusiano kwa Umma,
VETA Makao Makuu
S.L. P. 2849
Dar es Salaam
Tanzania
pr@veta.go.tz
Simu: 0625505027/0712259825/0712148332



No comments:

Post a Comment