Mahafali
ya kwanza ya mafunzo ya uwanagenzi yanayoendeshwa kwa ushirikiano kati ya VETA
, Chuo cha Humburg Germany na wenye viwanda yamefanyika leo kwenye chuo cha
VETA Dar es Salaam.
Mahafali hayo yamehusisha wanagenzi 48 wa fani za Umeme na Ufundi Magari.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo alikuwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Bw. Peter Maduki.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo alikuwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Bw. Peter Maduki.
Wageni wengine maalum waliohudhuria hafla hiyo ni aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Ufundi Humburg Bw.Frank Glucklich, Mshauri wa mradi Bw.Nicholaus Udewald, Mkurugenzi wa Mafunzo Bi.Leah Dotto na Mratibu wa Mradi, Mw. Francis Komba.
Mgeni rasmi Bw. Peter Maduki alisema baada ya mafanikio katika majaribio ya mradi, imedhihirika wazi kuwa mfumo huo wa mafunzo unazalisha wahitimu mahiri wanaoendana na mahitaji ya soko la ajira.
Alisema kuwa VETA inatazamia kupanua mafunzo hayo katika vyuo vyake mbalimbali na kuongeza kozi nyingine.
No comments:
Post a Comment