Mkurugenzi wa IYF Tanzania Joan Kimirei amesema kuwa vijana hao walipatiwa mafunzo ya ufundi stadi yaliyoenda sambamba na stadi za maisha na ujasiriamali ili kuwajengea uwezo wa kuanzisha miradi yao baada ya kuhitimu.
Kimirei amesema
hayo wakati wa warsha ya kujenga ufahamu kwa wadau wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi kuhusu
mradi wa Via: Jiandalie Ajira wa Shirika hilo uliofanyika mkoani morogoro
tarehe 15 hadi 16 Oktoba, 2020 na kuwashirikisha Wakurugenzi wa Kanda, Wakuu wa
Vyuo, Waratibu wa Mafunzo na Wakufunzi kutoka vyuo vya ufundi stadi.
Kimirei amesema pamoja na mambo mengine mradi huo, ulilenga kuwapatia vijana ujuzi na mafunzo ya ujasiriamali ili kukabiliana na tatizo la ajira.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt. Pancras Bujulu amesema
kuwa mradi huo umefungua mlango wa ajira kwa vijana na kwamba VETA itaendeleza
baadhi ya programme za mafunzo yaliyokuwa yakitolewa kupitia mradi, ikiwemo
kutumia mtaala wa KTS (Key To Success) kwenye kozi za muda mfupi.
Mradi wa Via: Jiandalie Ajira ulianzishwa mwaka 2018 na unatarajiwa umalizika mwaka huu 2020.
No comments:
Post a Comment