CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Sunday 30 May 2021

TRA YATOA MBAO KUSAIDIA UJENZI WA CHUO CHA VETA NEWALA

 

Ofisi ya Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Kusini Mashariki imepokea msaada wa mbao za mninga 300 kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa ajili ya kutengeneza Samani za chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Newala kinachojengwa katika eneo la Kitangali, wilaya ya Newala, mkoani Mtwara.

Makabidhiano hayo yamefanyika tarehe 26 Mei, 2021 kati ya Meneja wa TRA Mkoa wa Mtwara Naomi Mwaipola na Meneja wa Soko la Ajira wa Kanda ya VETA Kusini Mashariki Prosper Saki mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Danstan Kyobya na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara-Mikindani Kanali Emmanuel Mwaigobeko.

Msaada huo umetokana na ahadi iliyotolewa na Kamishna Mkuu wa TRA kusaidia Taasisi za Serikali mkoani humo wakati wa hafla ya kumuaga aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa huo Alphayo J. Kidata mwezi Aprili 2021

No comments:

Post a Comment