CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Wednesday 2 June 2021

VETA KATIKA MAONESHO YA PILI YA VYUO VYA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

 

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeshiriki Maonesho ya Pili ya Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwenye Viwanja vya Jamhuri, Jijini Dodoma, tarehe 27 Mei hadi tarehe 2 Juni 2021. Katika Maonesho hayo, VETA imewakilishwa na vyuo vyake vinavyotoa kozi zenye ithibati ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE). Vyuo vilivyoshiriki ni Chuo cha TEHAMA cha VETA Kipawa, Chuo cha VETA cha Hoteli na Utalii (VHTTI-Njiro, Arusha), Chuo cha Walimu wa Ufundi Stadi Morogoro (MVTTC) na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi na Huduma Dar es Salaam.

Mhandisi Frank Urio, Mkufunzi wa Kozi ya Umeme, katika Chuo cha Walimu wa Ufundi Stadi Morogoro (MVTTC), upande wa kulia, akitoa maelezo kwa  wananchi waliotembelea banda la VETA, juu ya matumizi ya mitambo ya kufundishia umeme (simulators) inayotumiwa na chuo hicho kuimarisha utoaji wa wa mafunzo kwa vitendo.


Mhandisi Frank Urio, Mkufunzi wa kozi ya Umeme, katika Chuo cha Walimu wa Ufundi Stadi Morogoro (MVTTC), upande wa kushoto, akitoa maelezo kwa  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe, juu ya matumizi ya mitambo ya kufundishia umeme (simulators) inayotumiwa na chuo hicho kuimarisha utoaji wa wa mafunzo kwa vitendo.


Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe (Kushoto, mbele) akisikiliza maelezo kutoka kwa Marynurce Kazosi, Mkufunzi wa kozi ya Afya na Lishe ya Chakula katika Chuo cha Hoteli na Utalii (VHTTI-Njiro, Arusha), kuhusu mafunzo yanatotolewa na chuo hicho kwenye kozi ya Uandaaji wa Chakula. Prof. Mdoe alitembelea banda la VETA kwenye Maonesho ya Pili Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, tarehe 29 Mei 2021.


Baadhi ya watu waliotembele banda la VETA kwenye Maonesho ya Pili ya Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwenye Viwanja vya Jamhuri, Jijini Dodoma wakifurahia vinywaji vilivyoandaliwa na Chuo cha VETA cha Hoteli na Utalii (VHTTI-Njiro, Arusha) ikiwa ni sehemu ya kuonesha umahiri wa walimu na wanafunzi katika eneo la huduma za hoteli na utalii.


Kulthumu Sato (kushoto), Mkufunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma Dar es Salaa, Fani ya Nguo na Ubunifu wa Mitindo ya Mavazi akieleza kuhusu mafunzo ya Fani ya Nguo na Ubunifu wa Mitindo ya Mavazi kwa watu waliotembelea banda la VETA kwenye Maonesho ya Pili ya Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma.


Farida Kondo Mkilalu, Mwanafunzi wa Chuo cha TEHAMA Cha VETA Kipawa akiwaelezea wananchi waliotembelea Maonesho ya Pili ya Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuhusu mfumo uliobuniwa na chuo chake kurahisisha uchakataji wa mauzo na faida katika biashara. 


Meneja Uhusiano wa VETA, Sitta Peter (katikati) akifanya mahojiano na wandishi wa habari kuhusu ushiriki wa VETA kwenye Maonesho ya Pili ya Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.


Marynurce Kazosi, Mkufunzi wa kozi ya Afya na Lishe ya Chakula katika Chuo cha Hoteli na Utalii (VHTTI-Njiro, Arusha), akifafanua kuhusu mafunzo ya chuo hicho kwa watu waliotembelea Maonesho ya Pili ya Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma.


Bellington Lyimo, Mbunifu wa Vifaa vya Maabara (katikati) akiwaonesha wanafunzi moja ya kifaa alichobuni kinavyofanya kazi katika kujifunza kwa vitendo.


No comments:

Post a Comment