CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Monday 7 June 2021

Waziri Mkuu Majaliwa aweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Chuo cha VETA Ruangwa

 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) leo, tarehe 7 Juni 2021 ameweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

Mradi huo unatekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa kusimamiwa na Mshauri Elekezi, Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), kwa gharama ya shilingi bilioni 2.2 kwa fedha za Mradi wa kukuza Ujuzi na Stadi za kazi (ESPJ)

Chuo hicho kitakapokamilika kitakuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi 560 kwa mwaka katika fani za ufundi umeme,  Useremala, Uungaji na Uchomeleaji vyuma, Uashi, Ushonaji na Mitindo ya Mavazi, Usindikaji Vyakula  na TEHAMA.

Kazi Inaendelea kukamilisha ujenzi wa vyuo vingine 30 vya ufundi stadi nchini.





No comments:

Post a Comment