Mradi wa ujenzi wa
Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Pangani mkoani Tanga umefikia asilimia 95
ya utekelezaji wake huku mafunzo yakitarajia kuanza kutolewa mwezi Januari,
2023.
Mradi wa Ujenzi wa Chuo hicho unatekelezwa na Chuo cha VETA Dar es Salaam kwa kutumia nguvu kazi ya ndani yaani Force Account.
Mradi huo unakadiriwa
kutumia takribani shilingi bilioni 2.8
hadi kukamilika kwake.
Chuo cha VETA Wilaya
ya Pangani kitatoa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana wa wilaya ya Pangani na
maeneo ya jirani ambapo vijana watapatiwa ujuzi kupitia fani mbalimbali na
hatimaye kuwawezesha kuajiriwa au kujiajiri kwenye shughuli mbalimbali za
kiuchumi ili kujipatia kipato na kuweza
kuendesha maisha yao na kukuza uchumi wa Wilaya ya Pangani na taifa kwa ujumla.
Ujenzi wa chuo hicho unajumuisha majengo kumi na saba (17) kama ifuatavyo: Karakana ya ushonaji, Karakana ya Kompyuta na uhazili, Kakarana ya ufundi wa magari na uchomeleaji vyuma, Karakana ya umeme na uashi, Jengo la Utawala( administration block), Madarasa mawili ( General class room), Bwalo la chakula na jiko, Nyumba ya Mkuu wa Chuo, Bweni la wasichana, Bweni la wavulana, Stoo, Jengo la jenereta, Vyoo vya watumishi, Vyoo vya wanafunzi wavulana, Vyoo vya wanafunzi wasichana na Kibanda cha ulinzi.
MWONEKANO WA MAJENGO KATIKA CHUO CHA UFUNDI STADI CHA WILAYA YA PANGANI
• Jengo la utawala( administration block)
• Kakarana ya ufundi wa magari na
uchomeleaji vyuma
• Karakana ya umeme na uashi
• Bwalo la chakula na jiko
• Nyumba ya Mkuu wa chuo
• Bweni la wasichana
• Bweni la wavulana
No comments:
Post a Comment