Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, ameikabidhi Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Stadi(VETA) vishikwambi 996 kwa lengo la kurahisisha mafunzo vyuoni hasa
katika eneo la Tehama.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo tarehe 4 Novemba, 2022 katika ukumbi wa Jiji la Dodoma uliopo Mtumba jijini Dodoma kwenye hafla ya uzinduzi wa ugawaji vishikwambi kwa walimu nchini.
Mhe. Majaliwa amezindua mpango huo ikiwa ni sehemu
ya mkakati wa Sera ya Taifa inayoakisi Mpango wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan
wa Maendeleo ya Taifa ya Awamu ya Tatu ulioanza mwaka 2020/2021 na unatarajiwa
kukamilika mwaka 2025/2026.
Mpango huu utawawezesha vijana walio vyuoni kupata
na kuzalisha ajira na kuongeza kasi ya teknolojia ambayo nchi inaiwekea mkazo
kwa sasa.
Hafla hiyo ya uzinduzi imehudhuriwa na viongozi
mbalimbali wa Chama na Serikali akiwemo Waziri wa Elimu na Sayansi na
Teknolojia, Mhe. Profesa Adolf Mkenda, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA
Anthony Kasore na Mkuu wa Chuo cha Ufundi Sradi na Huduma cha Mkoa wa Dodoma
Ndugu Stanslaus Ntibara.
No comments:
Post a Comment