Jumla ya vijana
4,000 katika mikoa ya Lindi, Manyara, Dodoma , Dar es salaam
wanatarajia kunufaika na mafunzo ya
ufundi Stadi kwenye fani za Ufundi Bomba wa Viwandani, Uchomeleaji na
Mekatroniki kwenye vyuo vya VETA kupitia mradi wa Ajira na Ujuzi kwa Maendeleo
ya Afrika(E4D).
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa VETA, Ndugu Felix
Staki, ambaye alikuwa akimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa VETA, alisema utekelezaji
wa mradi wa E4D utachangia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza udahili, kutoa
fursa zaidi kwa vijana kupata ujuzi kupitia mafunzo ya ufundi stadi, kuimarisha
ubora wa mafunzo ya ufundi stadi kupitia vifaa vya kisasa vya kufundishia
pamoja na kuongeza ujuzi kwa walimu wa ufundi stadi.
Alisema katika chuo cha VETA Lindi mradi huo unatarajia
kunufaisha vijana 700 watakaopata mafunzo ya muda mfupi kwenye fani za Ufundi Bomba
pamoja Uchomeleaji na Uungaji vyuma ambapo jumla ya shilingi 228 milioni
zimetumika kununulia vifaa.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bi Zainab Telack, alisema ni matarajio ya Serikali ya Mkoa kuwa vijana watakaohotimu mafunzo hayo watakuwa na ujuzi wa kutosha utakaowawezesha kujiajiri.
Naye Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA Lindi, Ndugu
Harry Mmari, alishukuru GIZ kwa vifaa vilivyotolewa ambavyo vitasaidia kutoa mafunzo na
kutengeneza ajira kwa vijana .
No comments:
Post a Comment