Serikali ya Finland
kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania umetoa ufadhili kwa mabinti 240 kupata
mafunzo ya ufundi stadi kupitia programu ya Chaguo Langu Haki Yangu.
Mabinti
wanaofadhiliwa ni wale wanaotoka kwenye mazingira magumu, ikiwemo waliofanyiwa
ukatili na kupewa mimba za utotoni na wenye ulemavu. Awamu ya kwanza ya utekelezaji
wa mradi huo ni katika Mikoa miwili ya Mara na Shinyanga katika Wilaya za
Kishapu, Kahama na Butiama.
Akizungumza jana,
tarehe 23 Machi 2023, wakati wa ufunguzi wa programu hiyo, Mkuu wa Wilaya ya
Kishapu, Mhe. Joseph Mkude, amewapongeza wadau hao kwa ufadhili walioutoa,
akisema mafunzo hayo yatawawezesha mabinti waliofadhiliwa kutimiza ndoto zao
zilizotaka kukatishwa kutokana na changamoto walizopitia.
Vilevile, Mhe. Mkude
alimshukuru Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa kutoa kipaumbele kwenye elimu na mafunzo ya ufundi stadi kwa kutoa
fedha kwa ajili ya kujengwa vyuo vya ufundi stadi VETA ngazi ya wilaya ikiwemo Wilaya
ya Kishapu.
Mkurugenzi wa Elimu
na Mafunzo ya Ufundi Stadi wa VETA, Ndugu Abdallah Ngodu
akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa VETA, amewaomba wadau hao kupanua zaidi
programu hiyo kwa kuwa VETA ina vyuo nchini kote, vikiwa na fani zipatazo 90.
“Tunaweza kutumia fursa ya vyuo hivi kuwapatia
mabinti wengi zaidi mafunzo kama haya, hasa kwa kuzingatia hali ya udahili wa
wasichana kwenye vyuo vya VETA kwa sasa bado ni ndogo ukilinganisha na
wavulana,” amesema.
Kwa upande wake
Mwakilishi wa Ubalozi wa Finland, Ndugu Juhana Lehtinen, amesema wamefarijika
kuona namna mabinti hao wanavyopata mafunzo ya ufundi stadi ambayo yanategemewa
kubadilisha mfumo wa maisha yao.
"Tumekuja hapa
VETA wilayani Kishapu kuona namna utekelezaji wa mradi wa Chaguo Langu Haki
Yangu unavyotekelezwa na kusaidia mabinti ambao wamefanyiwa ukatili na wengine
kupewa mimba za utotoni…nimefurahi kuona unatekelezwa vyema na mabinti wanapata
ujuzi," amesema
Naye Mshauri wa
masuala ya jinsia kutoka UNFPA ambao ni waratibu wa programu hiyo, Maya Hansen,
amewataka mabinti hao kutumia vyema fursa waliyoipata kuleta chachu ya
mabadiliko katika maisha yao na kutofanya changamoto walizopata mwanzo
kuwarudisha nyuma.
Mkurugenzi wa Shirika
la WILDAF Tanzania, Anna Kulaya, amesema kazi kubwa ya WILDAF ni kutetea haki
za wanawake na wasichana, hivyo programu hiyo imekuja wakati mwafaka na
itasaidia kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na
watoto kupitia ujuzi ambao utawasidia
kuendesha maisha yao bila utegemezi.
Mkuu wa Chuo cha VETA
Shinyanga, Ndugu Magu Mabelele, ambaye pia ni msimamizi wa Chuo cha VETA cha
Wilaya ya Kishapu, amesema walipokea mabinti 240 kupitia Shirika la WiLDAF
kutoka Hamashauri tatu za Wilaya za Kishapu, Kahama na Butiama na hivyo uongozi
wa chuo cha VETA Shinyanga ukaamua kuwagawa mabinti hao kutokana na fani
walizochagua ambapo mabinti 171 wanapata mafunzo katika fani za Ushonaji (101),
Ufundi Bomba (11), Saluni (37), pamoja Ufundi Umeme (22).
Wengine 69 wamesalia
katika chuo cha VETA Shinyanga ambapo wanasomea fani za Uhazili na Tehama (27),
Upishi (18), Uchomeleaji na Uungaji Vyuma (7), Ufundi wa Magari (3) pamoja
Udereva wa Magari na Mitambo
No comments:
Post a Comment