Leo tarehe 20 Machi,
2023, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore, amekabidhi magari saba
kwa Kanda na vyuo vya VETA ili kuboresha utekelezaji wa shughuli za utoaji
elimu na mafunzo ya ufundi stadi nchini.
Magari hayo yenye
thamani ya shilingi bilioni 1.19 yamekabidhiwa kwa Mkurugenzi wa VETA Kanda ya
Kaskazini na Wakuu wa vyuo vya VETA vya Kanadi, Ndolage, Ruangwa, Nyasa, Newala
na Ngorongoro.
CPA. Kasore amesema
kasi ya ukuaji wa Mamlaka hiyo inayotokana na ujenzi wa vyuo vipya na kupanuka
kwa shughuli za mafunzo kumepelekea ongezeko la uhitaji wa magari na kwamba jitihada mbalimbali
zimeendelea kufanyika ili kukidhi mahitaji hayo.
“Jitihada zinazofanywa na Mamlaka ni pamoja na kutenga bajeti kila mwaka wa fedha kwa ajili ya kununua magari mapya pamoja na kuomba magari kwa wadau mbalimbali,”amesema
Aidha, CPA Kasore
ameagiza Wakuu hao kuzingatia na kusimamia matumizi sahihi ya magari hayo na
kuhakikisha yanatunzwa na kufanyiwa matengenezo kwa mujibu wa taratibu
zilizowekwa.
Mkurugenzi wa
Rasilimali watu na Utawala wa VETA,Ndugu Felix Staki, amesema ugawaji wa magari
hayo katika awamu hii umezingatia umbali wa vyuo na maeneo ya upatikanaji wa
huduma mbalimbali za kijamii na kwamba vyuo vingine vitaendelea kupatiwa magari
hayo kadri yatakavyoendelea kupatikana.
No comments:
Post a Comment