Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA. Anthony
Kasore, amewataka wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa vyuo 25 vya ufundi stadi vya
wilaya unaotekelezwa na VETA kwa nguvukazi ya ndani (Force Account) kuweka
mpango kazi wa umaliziaji wa majengo ili ifikapo Aprili 2023 mradi uwe
umekamilika.
CPA Kasore ametoa agizo hilo baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyuo vya VETA vya wilaya ya Kwimba, Kishapu, Igunga, Ikungi na Bahi tarehe 11 na 13 Aprili 2023
Amesema, majengo hayo yanatakiwa kukamilika mwishoni
mwa mwezi Aprili, 2023 na hakutakuwa na muda wa nyongeza tena.
"Ninachotaka kuona ni kila chuo kuwa na mpango kazi utakaobainisha namna umaliziaji utakavyofanywa kwa kila jengo kwa kuzingatia kuwa kazi hii inatakiwa kukamilika katika kipindi kilichopangwa" Amesema.
CPA Kasore ameongeza kuwa angependa wakati kusherekea Siku ya Wafanyakazi-Mei Mosi iambatane na sherekea za makabidhiano ya vyuo hivyo.
CPA Kasore amesisitiza usimamizi wa karibu wa
mafundi wanaotekeleza ujenzi huo ili kuhakikisha viwango vinazingatiwa.
No comments:
Post a Comment