Utekelezaji wa mradi
wa ujenzi wa jengo la ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Stadi (VETA) umeanza rasmi leo, baada ya Mkandarasi kukabidhiwa eneo la
ujenzi lililopo Medeli jijini Dodoma.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo tarehe 24 Juni, 2023 baina ya kampuni ya ABECC Ltd ambaye ni Mshauri Elekezi aliyewakilishwa na Mkadiriaji Majenzi, Novatus Mikapagaro na Kampuni ya ujenzi MOHAMMEDI Builders Ltd aliyewakilishwa na Mhandisi Ujenzi, Josephat Loya, na kushuhudiwa na Menejimenti ya VETA ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wake, CPA. Anthony Kasore.
Ujenzi wa jengo hilo
litakalokuwa na miundombinu mbalimbali ikiwemo vyumba vya ofisi, maegesho ya
magari, kumbi za mikutano na maktaba unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha
miezi 12.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA. Anthony Kasore, amesema VETA itatoa ushirikiano utakaohitajika katika kufanikisha utekelezaji wa mradi huo na kuwasisitiza watekelezaji wa mradi kuhakikisha ujenzi unafanyika kwa ubora, ufanisi na kwa wakati kwa mujibu wa mkataba.
Wafanyakazi wa VETA
Makao Makuu walihamia jijini Dodoma mwaka 2021 ambapo wamekuwa wakitumia
majengo ya ofisi za VETA Kanda ya kati kutekeleza shughuli za Mamlaka hiyo.
No comments:
Post a Comment