Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, amesema Serikali itaendelea kutoa
kipaumbele kwenye mafunzo ya ufundi stadi na kuongeza fursa zaidi za watanzania
kujipatia mafunzo hayo.
Prof Mkenda ameyasema
haya jana tarehe 11 Julai, 2023 alipotembelea chuo cha VETA cha Mkoa wa Tanga
ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili jijiji hapo.
Akiwa chuoni hapo Mhe.
Mkenda amesema kwa sasa Serikali inajenga vyuo vya VETA kote nchini kuwezesha
wananchi wote wanaohitaji mafunzo hayo kuyapata bila kikwazo chochote.
“Napata mrejesho kutoka
kwa wananchi na ukweli ni kwamba
wamefurahi sana na wananipa shukrani nipeleke kwa Mheshimiwa Rais kwa uamuzi wa
kujenga VETA katika kila wilaya,”amesema
Prof Mkenda ameiagiza
VETA kujipanga vizuri kukidhi matumaini ya wananchi hasa kwa kuzingatia ubora
wa mafunzo yanayotolewa ili kuwezesha vijana kujipatia ujuzi unaokidhi mahitaji
ya soko la ajira.
Prof. Mkenda ameahidi
kuendeleza ziara zake kwenye vyuo vya VETA ili kujionea na kujiridhisha juu ya
mafunzo yanayotolewa na kuahidi kuzifanyia kazi changamoto zinazokabili utoaji
mafunzo.
Naye Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore, amesema katika mwaka wa fedha 2022/2023
Wizara imeitengea VETA kiasi cha shilingi billion 54 ambapo tayari
wameshapatiwa zaidi ya shilingi bilioni 49 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli
mbalimbali za Mamlaka hiyo.
CPA Kasore amemshukuru
Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa
kuhakikisha VETA inapata fedha za miradi mbalimbali hasa ya mafunzo ya ufundi
stadi ili kusogeza mafunzo hayo karibu na wananchi.
Pia aliishukuru
serikali kwa kutoa vibali vya ajira kwa watumishi wapatao 514 ambao wameongeza
tija katika mafunzo.
Katika ziara hiyo,
Waziri Mkenda alitembelea karakana katika chuo hicho na kupanda mti wa
kumbukumbu
No comments:
Post a Comment