CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Friday 15 September 2023

VETA Mshindi wa Kwanza Maonesho ya Siku ya Wahandisi

 

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeibuka Muoneshaji  Bora kwenye Kundi la Utafiti na Maendeleo kwenye Maonesho ya Siku ya Wahandisi Nchini (Annual Engineers Day) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam, tarehe 14 hadi 15 Septemba,

 2023.Kundi hilo lilihusisha ushindani wa Taasisi saba ambapo nafasi ya pili imechukuliwa na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mt. Joseph.


Kupitia maonesho hayo, VETA ilitoa elimu ya namna inavyoandaa nguvukazi kwa ajili ya kusaidia shughuli za Uhandisi na kuwahakikishia Wahandisi uwepo wa nguvu kazi mahiri na ya kutosha kwa ajili ya kutekeleza shughuli mbalimbali za kihandisi ikiwemo ujenzi wa majengo na miundombinu mbalimbali pamoja utekelezaji wa miradi ya kimkakati nchini.                 

Maonesho hayo yalifunguliwa jana, tarehe 14 Septemba 2023 na Mheshimiwa Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na yamefungwa leo, tarehe 15 Septemba 2023 na Mheshimiwa Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment