Mamlaka
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeihakikishia jamii utayari wake
katika utekelezaji wa mitaala mipya ya Sekondari kwa upande wa utoaji mafunzo
ya amali.
Meneja
Uhusiano wa VETA, Ndg. Sitta Peter, amesema hayo tarehe 3 Desemba, 2023,
wakati wa kuhitimisha maonesho ya miaka 50 ya NECTA yaliyofanyika katika
viwanja vya Mnazi Mmoja jijini, Dar es salaam.
Ametaja
baadhi ya majukumu ya VETA kwenye
utekelezaji wa mitaala hiyo kuwa ni kuandaa mitaala na vitabu vya kufundishia
mafunzo ya amali na kusimamia utoaji wa mafunzo hayo kwa ufanisi.
Amesema,
tayari VETA imeshaandaa mitaala, miongozo na vitini kwa ajili ya mafunzo ya
amali shule za sekondari, ambayo yanatarajiwa kuanza Januari, 2024.
Sambamba
na hilo ametoa wito kwa wahitimu wa darasa la saba na kidato cha nne kujipatia
ujuzi katika vyuo vya VETA nchini katika kipindi cha mpito wanachosubiria
kuendelea na hatua zingine za masomo.
Amesema
ujuzi huo utakuwa akiba kwenye maisha yao na kuwawezesha kujiajiri na
kuajiriwa.
No comments:
Post a Comment