CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Thursday 21 December 2023

Wajumbe wa Bodi Bodi ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET Board) watembelea kiwanda cha samani VETA Dodoma

Wajumbe wa Bodi ya Tisa ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET Board) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Prof. Sifuni Mchome, tarehe 21 Desemba, 2023 wametembelea kiwanda cha kutengeneza Samani cha VETA jijini Dodoma kujionea shughuli za uzalishaji samani zinavyoendeshwa kiwandani hapo.

Kabla ya ziara hiyo, wajumbe hao walikutana katika kikao maalum cha Bodi hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano VETA Makao Makuu jijini Dodoma kwa lengo la kujadili na kuweka mikakati mbalimbali inayolenga kuimarisha utoaji wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi nchini.

No comments:

Post a Comment