Walimu na wanafunzi katika chuo cha
VETA Wilayani Uyui, Mkoani Tabora, tarehe 28 Februari, 2024 wamepanda miti
zaidi ya 500 katika chuo cha VETA Wilaya ya Uyui.
Zoezi hilo lililokuwa na lengo la
kutunza mazingira na utekelezaji wa maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar limeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Mhe. Zakaria
Mwansasu ambapo pia Katibu Tawala wa Wilaya ya hiyo Bi Neema Mfugale
alihudhuria.
Akizungumza baada ya zoezi la
upandaji miti, Mhe. Mwansasu amesisitiza miti hiyo kutunzwa na kuagiza kila
mwanafunzi chuoni hapo kukabidhiwa mti kwa ajili ya kuutunza.
“Nakabidhi miti hii naomba kila shimo
liwe na mwanafunzi mmoja au wawili ili huo mti ukipotea au kukauka ni lazima
urudishiwe. Tusipande miti halafu kesho na keshokutwa miti hiyo inakauka,”
amesema.
Ameongeza, “Tunataka tupande miti hii
ili kesho na kesho kutwa tukirudi tunasema sisi ndio wanafunzi wa kwanza wa
chuo hiki tuliopanda miti hii,”
Naye Kaimu Msajili wa chuo hicho
,ndugu Fedric Phanuel Lukumay amewashukuru Wakala wa Misitu(TFS), Wilaya ya
Uyui na Mhifadhi wa wilaya, kwa kukubali
ombi lao la kuwapatia miti hiyo mia tano iliyopandwa chuoni hapo.
Amesema wamepanda miti katika chuo
hicho sio tu katika kutunza mazingira, lakini pia katika kuweka mandhari bora
na mipaka kuzunguka chuo hicho.
No comments:
Post a Comment