CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Friday 31 May 2024

WAZIRI MKUU AIPONGEZA VETA KWA BUNIFU ZENYE TIJA KWA JAMII



Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa(Mb) ameipongeza Mamlaka ya Elimu na Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kwa ubunifu  unaolenga kutatua changamoto zinazoikabili jamii.

Mhe. Waziri Mkuu ametoa pongezi hizo alipotembelea Banda la VETA, leo tarehe 31 Mei 2024, katika Kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Popatlal, jijini Tanga.

Akiwa katika banda hilo la VETA Waziri Mkuu Majaliwa, alijiionea ubunifu wa kifaa cha kuongeza usikivu kwa  watu wenye usikivu hafifu  na kifaa cha kudhibiti dereva kusinzia wakati akiendesha gari.

"Tumekuwa na watu wengi wanaosumbuliwa na tatizo la usikivu hafifu ambapo tukiwatumia VETA na wabunifu wao tunaweza kuzalisha vifaa vingi na vya kutosha ndani ya nchi vitakavyowasaidia badala ya kuagiza kutoka nje" amesema.

Naye ndugu Innocent Maziku, Mwalimu na mbunifu wa kifaa hicho cha kuongeza usikivu kwa watu wenye usikivu hafifu kutoka chuo cha VETA Kigoma ameahidi kutoa ushirikiano kwa Mamlaka husika katika kusaidia kuzalishwa/kutengenezwa kwa vifaa hivyo kwa wingi ili kuwasaidia Watanzania wengi wenye tatizo hilo.

Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yaliyoanza rasmi tarehe 25 Mei, 2024 yamekifia kilele na kufungwa  rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo tarehe 31 Mei, 2024



No comments:

Post a Comment