CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Wednesday 5 June 2024

Mkoa wa Tabora waadhimisha Siku ya Mazingira Duniani kwa kupanda miti 120 chuo cha VETA Uyui

 

Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani mkoani Tabora yamefanyika leo tarehe 5 Juni 2024 katika chuo cha VETA Uyui, ambapo zoezi la kupanda miti limefanyika chuoni hapo.

Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Mhe. Zacharia Mwansansu ameongoza zoezi hilo la upandaji miti akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambapo jumla ya miti 120 imepandwa chuoni hapo.

Madhimisho hayo yenye kauli mbiu isemayo "Urejeshwaji wa Ardhi, ustahimilivu wa hali ya Jangwa na Ukame" yana lengo la kutoa elimu ya utunzaji na uhifadhi wa Mazingira.




No comments:

Post a Comment