Watumishi wa VETA Makao
Makuu wamepewa mafunzo ya kupambana na majanga ya moto ikiwa ni sehemu ya
juhudi za Mamlaka kuhakikisha usalama mahala pa kazi.
Mafunzo hayo
yametolewa tarehe 31 Mei, 2024 katika eneo la VETA Makao Makuu,
jijini Dodoma na kuwasirikisha watumishi wa idara na vitengo vyote vya VETA.
Akitoa mafunzo hayo ya
kupambana na majanga ya moto, Insp. Stephen Katte kutoka Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji, mkoani Dodoma amesema majanga ya moto yanaepukika kama wananchi
wataweka mkazo katika utayari, umakini na uelewa wa kinga na matumizi ya vifaa
vya kuzimia moto.
Hata hivyo Insp.
Katte amewataka wananchi kuwa na utamaduni wa kupeleka ramani za majengo yao
kwa jeshi lazima moto ili zifanyiwe ukaguzi kabla ya kuanza ujenzi.
“kwasasa tumejikita
katika kuzuia majanga ya moto ndio maana tunashauri utuletee ramani ya nyumba
kabla ya kuanza ujenzi ili tuweze
kuipitia na kuona kama ina mifumo ya
kung’amua dalili za moto au moshi,” amesema
Insp. Katte.
Kwa upande wake FC
Jegu Donias nae kutoka Jeshi la Zimamoto
na uokoaji mkoani Dodoma ameshauri wananchi kuacha kutumia "cable"
moja kwa matumizi ya vifaa vinavyotumia umeme kama vile jokofu, feni, runinga,
kuchaji simu kwa wakati mmoja.
Ameongeza kuwa ili kujikinga na majanga ya moto ni vimema
maeneo ya ofisini, nyumbani na kwenye mikusanyiko ya watu wengi kama
sokoni kufungwe vifaa vya kukabiliana na moto.
Sambamba na hilo FC Donias ameelezea mambo ya kufanya Unapogundua moto.
Amesema jambo la
kwanza unatakiwa kupiga king’ora, kengele au mayowe ili kuashiria kwamba kuna
tukio lisilo la kawaida na kuita Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kupitia namba ya
dharula 114.
Furaha Paul ambaye ni
Kaimu Meneja Miliki VETA ameshukuru Jeshi la Zimamoto na ukoaji kwa kutuoa
mafunzo hayo kwa watumishi wa VETA Makao Makuu na kuwapongeza watumishi wa VETA
kwa kushiriki mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment