CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Friday 5 July 2024

Mafundi nguo wenye ulemavu wapata dili Sabasaba

 

Kuona ni kuamini ndivyo unavyoweza kusema kutokana na umahiri unaooneshwa na vijana wenye ulemavu waliohitimu fani ya ushonaji, ubunifu na teknolojia ya nguo kutoka vyuo vya Veta ambao wamepata fursa ya kuwashonea washiriki na watembeleaji wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu Sabasaba.

Vijana hao Riziki Ndumba na Abdi Kipara wenye ulemavu wa viungo ambao wako katika banda la Mamlaka ya Ufundi Stadi (VETA) mbali ya kueleza namna walivyonufaika na mafunzo pia wameweza kuaminiwa na baadhi ya washiriki na watembeleaji wa maonesho hayo kwa kuwashonea nguo na kujiongezea kipato. Soma zaidi. 

 Chanzo: mtanzania.co.tz


No comments:

Post a Comment