CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Tuesday, 20 August 2024

VETA, ENABEL KUWEZESHA VIJANA KUPATA UJUZI, KUTUNZA MAZINGIRA

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) na Shirika la Maendeleo la Ufalme wa Ubelgiji (ENABEL)  zimesaini Hati ya Mashirikiano kwa lengo la kuboresha kuwezesha vijana kupata ujuzi na kushiriki katika utunzaji mazingira.

Makubaliano hayo yametiwa saini, tarehe 19 Agosti 2024, katika ukumbi wa Hotel ya Protea, Jijini Dar es Salaam na Wakurugenzi Wakuu wa taasisi hizo.

Makubaliano yatahusisha  utekelezaji wa miradi miwili itakayotekelezwa  katika vyuo vya VETA Kipawa, Mwanza, Tanga, Kasulu, Kigoma na Buhigwe.

Akizungumza katika hafla hiyo ya kutiliana saini, Mkurugenzi Mkuu wa Enabel nchini Tanzania, Ndugu Koenraad Goekint alisema, shirika lake limewalenga zaidi vijana wa kike kwa kuwapatia ulinzi na usawa wa kijinsia, kuwapatia elimu na ujuzi na kutafuta fursa za kazi.

“Wasichana na wanawake vijana wenye umri wa miaka 14 hadi 19 watawezeshwa kupata elimu ya ufundi stadi kwa kushirikiana na VETA, kuwatafutia ajira na kuwaongezea fursa za kujiajiri,"  Koenraad amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore, ameitaja miradi itakayotekelezwa ni "Wezesha Binti" na "Elimu ya Utunzaji Mazingira."

Amesema, Wezesha Binti ambao unalenga kuwawezesha  mabinti kupata elimu ya Ufundi Stadi ili waweze kuajiriwa na kujiajiri utatekelezwa Kigoma Mjini na Kasulu. 

Ameongeza kuwa mradi wa elimu ya kutunza mazingira utatekelezwa katika mikoa ya Tanga na Mwanza na vijana watapewa mafunzo kuhusiana na ujuzi wa kutunza miundombinu ya mazingira na kuweza kushiriki katika shughuli za kiuchumi.




No comments:

Post a Comment