Timu
ya mpira wa miguu VETA Makao Makuu imeendelea kuonesha ubabe katika michezo ya
kirafiki inayofanyika ikiwa ni mwendelezo wa maandalizi ya ushiriki kwenye
mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma,Taasisi na Makampuni
Binafsi ( SHIMUTA).
Jana, Ijumaa, tarehe 13 Septemba 2024, VETA Makao Makuu imejinyakulia ushindi wa goli 1-0 dhidi ya timu ya Tume ya Utumishi wa Umma katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye viwanja vya Killimani Uzunguni, jijini Dodoma.
Katika
mchezo huo ambao ulikuwa wa aina yake, timu zilienda mapumziko zikiwa
hazijapata kitu, licha ya nafasi nyingi kutengenezwa.
Kipindi
cha pili kilianza huku timu zote zikionesha kuhitaji ushindi kwenye mchezo huo,
VETA ikapata bao kupitia kwa Juma Nassari na kuwainua mashabiki wa VETA.
No comments:
Post a Comment