Mamlaka ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeendaa semina ya kuwajengea uwezo Maafisa
Udhibiti Ubora kutoka Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar (VTA) ili kuimarisha utendaji wao.
Akizungumza katika ufunguzi wa semina hiyo, jana, tarehe 11 Septemba 2024, Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Dkt. Abdallah Ngodu, amesema semina hiyo ni ya siku tatu, ambapo maafisa kutoka VTA watapitishwa katika miongozo mbalimbali ya udhibiti ubora na viashiria vya ubora katika utoaji na usimamizi wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi au mafunzo ya amali.
“Kimsingi tumekuja
kuchangia uzoefu (VETA) tulionao”, Dkt. Ngodu amefafanua.
Mkaguzi Mkuu wa Vyuo
na Vituo vya Mafunzo ya Amali Zanzibar (VTA), Mhandisi Ibrahim Haji, amesema
Maafisa Uthibiti Ubora kutoka VTA wana lengo la kujifunza kutoka VETA namna
bora ya kufanya kaguzi ili kuboresha utendaji kazi na kufanya mafunzo ya ufundi
amali yabaki kwenye ubora uliokusudiwa.
No comments:
Post a Comment