Mamlaka ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi stadi (VETA) pamoja na Mamlaka ya Elimu ya Mafunzo ya Amali
Zanzibar (VTA), jana, tarehe 6 Januari 2025, wamekutana katika ukumbi wa
mikutano VETA Makao Makuu, jijini Dodoma kwa dhumuni la kujadiliana juu mambo ya kupendekeza katika maboresho ya
sheria ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya
Amali Zanzibar.
Mkurugenzi wa VTA, Dtk Bakari Silima amesema uboreshaji huo wa sheria unahusiana na uundwaji wa Mamlaka ya Uthibiti wa vyuo vya Amali vya serikali na binafsi na sheria nyingine itakuwa ya kuunda Taasisi ya kuendeleza vyuo vya amali vya serikali.
“Hivi sasa tupo katika hatua ya kuandaa rasimu mbili za kisheria ili kutenganisha baina ya jukumu la usimamizi na udhibiti ubora wa mafunzo ya amali na jukumu la utoaji wa mafunzo kama ilivyo hivi sasa hapa Tanzania Bara, hivyo tumeona ni jambo muhimu kushirikiana nanyi (VETA);katika kuboresha sheria hizo kwani tuna amini nyinyi mnauzoefu wa muda mrefu" amsema Dkt Silima.
Kwa upande wake Mkurugenzi
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi wa VETA Dkt Abdallah Ngodu
akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa VETA, amepongeza VTA kwa hatua madhubuti
walizo chukua na kuamua kuishirikisha Menejimenti ya VETA katika mchakato huo
wa uboreshaji sheria ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Amali Zanzibar.
Aidha Dkt Ngodu ameleza majukumu ya VETA kisheria kwasasa yamebaki manne.
“Ifahamike kwamba majuku ya VETA kisheria ni haya kuratibu,kukuza Elimu na mafunzo ya ufundi stadi, kusimamia mfuko wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi na uandaaji mitaala" amesema Dkt Ngodu.
Mamlaka ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Amali ilianzishwa
chini ya Sheria ya Mafunzo ya Amali mwaka 2005 ikiwa na majuku ya
kupanga,kusimamia,kudhibiti(kurekebu),kuratibu, kuendeleza na kutoa Mafunzo ya
Amali Zanzibar.
No comments:
Post a Comment