“Kwenye eneo la teknolojia kwanza kabisa hatuwezi kukataa siku hizi teknolojia imekuwa kwa kasi zaidi na kama tunavyoona siku hizi kwenye viwanda vingi wanahitaji matumizi ya robot kufanya kazi zao na kuna mashine ambazo zipo na teknolojia ya hali ya juu sasa sisi kama veta tumekuwa tukijitahidi kuhakikisha tunaendana na kasi ya teknolojia kwa kutoa mafunzo ambayo ni ya kiteknolojia ili kuhakikisha mwanafunzi anaemaliza aendane na soko la ajira.
Sisi kama veta tulikuwa na mpango wakuongeza
wataalamu zaidi ya 1000 na mpaka sasa tumeshaajiri wataalamu 600 ambao wamekuwa
wakufunzi kwenye vyuo vyetu nchi nzima na kwa kufanya hivyo tunataka kutoa
wanafunzi ambao akishamaliza chuo ataweza kuajiriwa au kujiajiri” - CPA Antony
Kasore - Mkurugenzi mkuu VETA
No comments:
Post a Comment