Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya, leo Jumanne, 27 Septemba, 2017 amezindua
Awamu ya pili ya Mradi wa Kuongeza Sifa za Kuajirika Kupitia Mafunzo ya Ufundi
Stadi (EEVT) katika Mikoa ya Mtwara na Lindi.
Uzinduzi huo umefanyika katika Chuo
cha VETA Mtwara
Katika Mradi huo makampuni ya Mafuta na Gesi chini ya
mwamvuli wa mradi wa Kuchakata Gesi Asilia (TLNG) unaojumuisha BG/Shell, ExonMobil, Ophir Energy, Pavilion Energy, na Statoil, yametoa kiasi cha Dola za
Kimarekani milioni 1.9, karibu sawa na Shilingi za Kitanzania bilioni 4, ili kuendeleza mradi wa
Kuongeza Uwezo wa Kuajirika, hususani kwa vijana wa mikoa ya Lindi na Mtwara.
Kiasi hicho cha fedha kitatumika katika kutekeleza
Awamu ya pili Mradi wa Kuongeza Sifa za Kuajirika Kupitia Mafunzo ya Ufundi
Stadi (EEVT) utakaotekelezwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi
(VETA), Shirika la Kimataifa la Huduma za Kujitolea (VSO) na Shirika la
Maendeleo la Ujerumani (GIZ) kupitia mpango wake wa Kuendeleza Ujuzi katika
Sekta ya Mafuta na Gesi (SOGA).
Mradi wa EEVT unalenga katika kuboresha uwezo wa kuajirika kwa vijana wa mikoa ya Mtwara na Lindi, kwa kuzingatia kuongezeka kwa mahitaji nguvukazi yenye ujuzi katika sekta ya uziduzi (extractive industry) ikijumuisha uchimbaji madini, gesi na huduma zinazoendana na maeneo hayo.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa Mhandisi Stella Manyanya
alizindua rasmi awamu ya pili ya mradi huo katika hafla iliyofanyika kwenye
chuo cha VETA Mtwara jana (Jumanne, Septemba 27, 2016).
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi, mwakilishi wa TLNG, Bi.
Kate
Sullam alisema kuwa mashirika hayo yameamua kutoa ufadhili wa awamu ya pili ya
mradi baada ya kuona mafanikio makubwa yaliyopatikana katika awamu ya kwanza ya
mradi uliotekelezwa na VSO and VETA kupitia vyuo vya VETA Mtwara na Lindi,
mwaka 2012 hadi 2015
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya aliwashukuru TLNG na wadau wote katika juhudi zao za kusaidia kuendeleza ujuzi nchini na kuwaomba makampuni mengine kuingia kwenye mradi huo kwani utawanufaisha pia wao kwa kuwapatia nguvukazi yenye ujuzi, hivyo kuongeza tija katika makampuni yao.
Aliwaasa
wakazi wa mikoa ya Mtwara na Lindi kushiriki kwa kujiunga katika mafunzo ya
ufundi stadi ili waweze kunufaika vyema na fursa za ajira zinazozidi kuongezeka
katika ukanda wa Kusini mwa Tanzania kutokana na kuongezeka kwa uwekezaji
unaochangiwa na kugundulika kwa gesi asilia.
“Mafunzo ya ufundi katika nchi nyingi yamekuwa chachu ya
maendeleo endelevu. Nchi nyingi zilizoendelea zinatilia mkazo elimu na mafunzo
ya ufundi stadi. Nchi kama Japani haina rasilimali za asili lakini iliwekeza
katika rasilimali watu na kuwa nchi ya pili duniani kiuchumi,” alisema.
Kaimu Mkurugenzi Mkuuwa VETA, Bw.
Geoffrey Sabuni alisema kuwa Mradi alisema kuwa Mradi wa EEVT ni miongoni mwa
miradi ya kipekee katika kusaidia VETA kufikia Malengo Namba 1 na 2 ya Mpango
Mkakati wa Nne wa VETA ambayo yanahusu Kupanua Fursa za Upatikanaji wa Mafunzo
ya Ufundi Stadi na Kuongeza Uwezo wa Kuajirika kwa Wahitimu wa Ufundi Stadi.
Akiwasilisha
kuhusu Mradi, Mkurugenzi wa Mafunzo wa VETA, Bi. Leah Dotto alisema kuwa awamu
ya kwanza ya mradi imewanufaisha wanafunzi 477 wakiwemo wasichana 103 na
wavulana 374, idadi ambayo ni zaidi kwa kiasi kikubwa kuliko lengo la awali la
mradi ambalo lilikuwa kufikia vijana 280.
Alitaja
mafanikio mengine ya kujivunia kutokana na mradi huo kuwa ni pamoja na kuongeza
uwezo wa vijana kuajirika kwa urahisi ambapo zaidi ya asili 51 ya wahitimu wa
ufundi waliokuwa kwenye mradi huo walipata ajira ndani ya miezi sita baada ya
kuhitimu na asilimia 93 waliweza kupata vyeti vya kutambulika kimataifa baada
ya kufaulu mitihani ya Taasisi
ya City and Guilds ya Uingereza.
Alisema
kuwa awamu ya kwanza ya mradi ilihusisha fani sita ambazo ni Uchomeleaji na
Uungaji Vyuma, Useremala, Ufundi Bomba, Umeme, Utayarishaji wa Chakula na
Ufundi Magari..
Alisema,
awamu ya pili itaongeza fani tatu mpya ambazo ni
Ujengaji wa majukwaa (Scaffolding and Rigging), Upakaji rangi viwandani
(Industrial painting) na Uendeshaji wa mitambo mizito (Heavy duty Equipment
Operation) kwa kuzingatia mahitaji ya soko la ajira hususan sekta ya gesi na
mafuta.
“zaidi ya
wanafunzi 550 wanatarajiwa kunufaika na mradi kwa kupata ujuzi unaotambulika
kimataifa; zaidi ya walimu 30 watapata mafunzo mafunzo maalum; zaidi ya
wanafunzo 105 watafundishwa juu ya mfumo wa Pasi ya Afya na Usalama kazini na
hatimaye kutunukiwa pasi za kimataifa za Afya na Usalama Kazini; na zaidi ya
makampuni 30 yanatarajiwa kuingia kwenye mradi kupitia kutoa fursa za mafunzo
kiwandani, jambo ambalo ni kitovu cha awamu ya pili ya mradi,” alisema.
No comments:
Post a Comment