Vijana wa Mkoa wa Simiyu wameonesha nia ya kujiunga na mafunzo ya ufundi stadi huku wakiamini kuwa elimu hiyo itawasaidia katika kujikwamua kimaisha na kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira.
Vijana
hao wameeleza nia hiyo wakati walipotembelea banda la VETA katika maonesho ya
wiki ya vijana yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba wilayani Bariadi.
Vijana
hao wanaamini kuwa elimu na mafunzo ya ufundi stadi ni muhimu sana katika
kuelekea nchi ya viwanda kwa kuwa viwanda vingi vidogo na vikubwa vitahitaji
vijana wenye ujuzi katika kuviendesha.
Linda
Noel (23) mkazi wa wilaya ya Meatu mkoani Simiyu amewataka vijana wenzake
kuhakikisha wanajipatia stadi mbalimbali zitakazowasaidia kuajiriwa na
kujiajiri huku akiiomba serikali kuharakisha ujenzi wa chuo cha VETA mkoani
hapo.
“Nawahamasisha
vijana wenzangu kujipatia stadi za ufundi ili waweze kuzitumia katika
kuchangamkia fursa mbalimbali kwenye maeneo yao,” Alisema.
Naye
Mkurugenzi wa Mafunzo – VETA Leah Dotto Lukindo alisema kuwa mamlaka inaendelea
na juhudi mbalimbali za kupanua wigo wa utoaji elimu na mafunzo ya ufundi stadi
pamoja na kuhamasisha vijana kujifunza stadi mbalimbali ili kuwa na nguvu kazi
ya kutosha kuhudumia viwanda na hata kuanzisha viwanda vidogo vidogo.
Mkurugenzi
huyo aliwataka wananchi, hususani
vijana kutambua kuwa elimu na mafunzo ya ufundi stadi ni nyenzo muhimu katika
kusukuma mbele maendeleo ya viwanda.
Mwalimu
wa VETA Shinyanga Yona Mwambopa akitoa elimu juu ya uongezwaji thamani madini
ya vito kwa kuyakata na kuyang`arisha wakati wananchi hao walipotembelea banda
la VETA katika maonesho ya Wiki ya Vijana mkoani Simiyu. Fani ya Ukataji na
Ung`arishaji wa madini ya vito inafundishwa katika chuo cha VETA Shinyanga.
Wananchi
mbalimbali wakipata maelezo kuhusu elimu na mafunzo ya ufundi stadi walipotembelea
banda la VETA katika maonesho ya wiki ya vijana mkoani Simiyu.
Mkurugenzi
wa Mafunzo- VETA Leah Dotto Lukindo akitoa mada juu ya mchango wa Elimu na
Mafunzo ya ufundi stadi katika kufikia Tanzania ya viwanda wakati wa kongamano
la vijana lililofanyika mkoani Simiyu wakati wa maadhamisho ya wiki ya vijana.
Wananchi
mbalimbali wakipata maelezo juu ya matumizi ya mashine ya kutambua matatizo ya
gari kutoka kwa mwalimu wa fani ya Ufundi wa magari katika Chuo cha VETA VETA Shinyanga.
Mwalimu
wa fani ya saluni na mapambo kutoka chuo cha VETA Shinyanga Siana Nkya akitoa
huduma kwa wananchi waliofika katika banda la VETA.
No comments:
Post a Comment