Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa VETA Ndugu, Geoffrey Sabuni (mbele kulia) pamoja na Petula
NashMkurugenzi wa IYF Nchini Tanzania (mbele kushoto) wakisaini Makubaliano ya
Mradi wa VIA Jiandalie Ajira kwenye ofisi za VETA Makao Makuu, Jumanne,
tarehe 1 Novemba, 2016. Mradi huo una lengo la kuwasaidia Vijana wanaoishi
kwenye mazingira magumu wapatao 22,550 kwenye
mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Mtwara kwa kuwapatia Mafunzo ya Ufundi stadi,
Stadi za Ujasiriamali na Maisha na ili hatimaye waweze kuwa na umahiri wa
ushindani kwenye soko la ajira. Nyuma waliosimama wakishuhudia ni Josephine
Meela kutoka IYF na Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ufundi Stadi –VETA, Leah Dotto
(kulia).
Mradi
huo ulizinduliwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhandisi
Stella Manyanya katika ukumbi wa Julius Nyerere uliopo jijini Dar
es salaam Tarehe 28/10/2016.
Mradi
huu ni unatekelezwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kwa
ushirikiano na shirika la International Youth
Foundation (IYF) na umefadhiliwa na MasterCard Foundation.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa VETA ndugu Geoffrey Sabuni na Petula Nash Mkurugenzi wa IYF
Nchini Tanzania wakipeana mkono wa pongezi mara baada ya
kusaini Makubaliano ya Mradi wa Via-Jiandalie
Ajira;
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa VETA Ndugu Geoffrey Sabuni pamoja na Petula Nash Mkurugenzi wa IYF Nchini
Tanzania wakijadiliana mambo mbalimbali
kuhusu mradi mara baada ya kusaini makubaliano.
No comments:
Post a Comment