Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dr Bwire S. Ndazi amefanya ziara katika
kanda na chuo cha VETA Dar es Salaam ambapo ametembelea karakana na
kufanya mazungumzo na wafanyakazi.
Katika ziara hiyo pamoja mambo mengine Dr Bwire amesisitiza juu ya suala la usalama kwenye karakana za mafunzo.
Katika ziara hiyo pamoja mambo mengine Dr Bwire amesisitiza juu ya suala la usalama kwenye karakana za mafunzo.
Dr Bwire alisema ipo haja ya kuhakikisha kuwa walimu na wanafunzi wote
wanapokuwa kwenye karakana wanavaa vifaa vya usalama vinavyohitajika
kulingana na fani husika.
“
Tunapaswa kuhakikisha masuala ya usalama katika karakana yanazingatiwa
ili wanafunzi wetu waone ni suala muhimu katika masomo yao na kuweza
kujenga utamaduni huo tangu wanapoingia chuoni” Alisema Dr Bwire
aliagiza uongozi na waalimu wa vyuo vya VETA kuhakikisha kuwa suala hilo
linapewa uzito wa hali ya juu kwa kuwa lina umuhimu mkubwa katika
utoaji wa mafunzo ya ufundi stadi na kwenye viwanda.
Alitaka
uongozi wa vyuo kwa kushirikiana na waalimu kuweka utaratibu wa
kuwazuia wanafunzi wasiokuwa na vifaa vya usalama kutoingia katika
karakana ili kuweza kuonesha umuhimu wa suala hilo.
Aliwasisitiza wafanyakazi kujiendeleza kimasomo kupitia programu mbalimbali za mafunzo ikiwemo mafunzo ya muda mfupi na yale yanayotolewa baada ya kazi.
Mkurugenzi
Mkuu pia aliwataka wafanyakazi wote kufanya kazi kwa kujituma na kwa
ushirikiano huku wakitambua kuwa wanayo dhamana kubwa ya kuwatumikia
watanzania kwa kuhakikisha utoaji na usimamizi bora wa elimu na mafunzo
ya ufundi stadi
Awali, Kaimu Mkurugenzi wa kanda
ya Dar es Salaam Winfred Camil aliwasilisha taarifa ya kanda hiyo na
kuzitaja changamoto mbalimbali ikiwemo uchakavu wa karakana na kujengea
uwezo waalimu ili kuboresha utoaji wa mafunzo kwa kuzingatia mabadiliko
ya teknolojia.
Katika kuhakikisha uboreshaji wa utoaji mafunzo,
Kaimu mkurugenzi Mkuu alionesha umuhimu wa VETA kupitia kanda na vyuo
vyake kutengeneza mashirikiano zaidi na viwanda ili kuwa na uelewa wa
teknolojia mbalimbali zinatotumika na hatimaye kuandaa nguvu kazi mahiri
itakayokidhi mahitaji ya soko la ajira
No comments:
Post a Comment