Mamlaka
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kwa kushirikiana na kampuni ya simu
za mkononi ya Airtel kupitia application ya VSOMO wametangaza na kuzindua
kozi mpya za ufundi stadi za VETA zitakazotolewa kupitia simu za mkononi ili
kuwawezesha watanzania kujiunga na kupata utaalamu na vyeti vya VETA kwa
gharama nafuu.
Alisema
mradi wa VSOMO unaisaidia VETA kutekeleza lengo la kupanua wigo wa utoaji
mafunzo na kuweza kuwafikia makundi yote katika jamii, kama inavyoainishwa
katika Mpango Mkakati wake.
Mkurugenzi
wa VETA Kanda ya Dar es Salaam Habib Bukko alisema VSOMO imekuja wakati ambao
serikali inaelekea kwenye uchumi wa viwanda na kwamba jamii inahitaji stadi
stahiki ili kuweza kufanikisha azma hiyo.
Awali,
Mkuu wa Chuo cha VETA Kipawa Eng. Lucius Luteganya ambaye ni Mratibu Mkuu wa
mradi huo alisema wakati wa uzinduzi wa mfumo huo wa mafunzo kwa njia ya simu
kupitia application ya VSOMO mwezi Juni 2016, mafunzo yalianza kutolewa katika
kozi za Ufundi umeme wa manyumbani, Ufundi pikipiki, Ufundi wa simu za mkononi,
Ufundi Alluminium, Utaalamu wa maswala ya urembo pamoja na Ufundi wa kuchomea
vyuma.
Aliongeza
kuwa, mfumo huu wa masomo kwa njia ya simu-VSOMO, sasa ni maarufu kwa vijana
ambapo takwimu zinaonyesha zaidi ya vijana 30,000 tayari wamepakua application
ya VSOMO, 8000 wamejiandikisha na kati yao 50 wanasoma kozi mbalimbali na wengine
tayari wameshahitimu na kupata vyeti vya VETA.
“ili
kupata mafunzo ya VSOMO unatakiwa kuwa na mtandao wa Airtel kisha pakua
application ya VSOMO katika google play store, na kujisajili na kisha chagua
kozi inayokidhi mahitaji yako,” Alisema
Eng.
Luteganya aliongeza kuwa katika kuhakikisha elimu inayotolewa inakidhi viwango
vya elimu vilivyowekwa na VETA, wanaofaulu masomo ya nadharia kupitia VSOMO
hupaswa kuhudhuria mafunzo ya vitendo katika vituo vya VETA vilivyopo maeneo
mbalimbali nchini.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya
alishukuru kwa VETA kuongeza kozi katika mfumo wa VSOMO.
“tunajisikia
furaha kuongeza kozi nyingi zaidi katika mfumo huu wa masomo kwa njia ya
mtandao wa VSOMO,kwani itatuwezesha kufikia idadi kubwa ya vijana wanaosoma kwa
kupitia simu zao za mkononi. Lengo letu ni kuhakikisha tunakuwa na kozi nyingi
ili kwenda sambamba na matarajio na mahitaji ya wanafunzi na watanzania kwa
ujumla,” alisema
No comments:
Post a Comment