Mafunzo
kwa njia ya simu yamebuniwa na VETA kwa kushirikiana na Airtel kwa lengo la
kupanua wigo wa mafunzo ya ufundi stadi na kurahisishia watu wengi kujifunza na
kupata ujuzi.
Mafunzo
haya kwa sasa yanahusisha kozi za muda mfupi.
Utaratibu
wa mafunzo umegawanyika katika sehemu mbili:
1.
Mafunzo ya nadharia ambayo hutolewa kupitia simu za mkononi-Simu za
kupangusa-smartphone.
2.
Mafunzo kwa vitendo ambayo hutolewa katika vyuo vya VETA.
Mlolongo
wa mafunzo ni kuwa, mtu anayetaka kujiunga huanza kwa kupakua application ya
VSOMO kwenye google play store( http://airtelfursa.com/vsomo/.) Kisha hujisajili kwa kutumia namba ya Airtel na
kuchagua aina ufundi/ujuzi anaotaka kujifunza.
Katika
simu yake atapata notice na kujisomea. Baada ya kujisajili anaweza kusoma
notice hata kama hayuko kwenye mtandao wa internet. Internet inahitajika wakati
wa kujisajili tu.
Mwisho
wa kila hatua-module, kuna majaribio na mitihani ambayo unapaswa kuifanya na
kufaulu kabla ya kuhamia kwenye hatua nyingine. Mitihani husahihishwa kwa mfumo
wa kompyuta. Ikiwa hujafaulu, mfumo utakuzuia kuendelea hatua inayofuata hadi
ufaulu.
Baada
ya kukamilisha hatua zote na kufaulu mitihani yote ya nadharia kwenye simu,
mwanafunzi hutakiwa kuchagua chuo cha VETA kilicho karibu naye au kile
anachopenda kwenda kufanya mafunzo kwa vitendo. Mfumo humtaarifu na kumpa
orodha ya vyuo vilivyopo ili ajaze na kufanya booking ya mafunzo ya vitendo.
Mfumo
wa kompyuta hutoa pia taarifa kwenye chuo juu ya wanafunzi wanaotarajiwa kufika
kwa ajili ya mafunzo ya vitendo.
Mwanafunzi
afikapo chuoni hufanyishwa kwanza mtihani wa majaribio ili kuhakikisha kama
kweli ni yeye aliyekuwa akisoma kwenye simu. Baada ya kufaulu mtihani huo ndipo
huanza rasmi mafunzo kwa vitendo.
Mwanafunzi
hukaa katika mafunzo ya vitendo kwa walau wiki mbili na kila siku hutakiwa
kutumia walau masaa 6 akijifunza kwa vitendo. Kwa hivyo baada ya wiki mbili
anakuwa amekamilisha masaa ya mafunzo ya vitendo yapatayo 60.
Hatimaye
hupewa mtihani wa mwisho na akifaulu hutunukiwa cheti.
Dah mfumo nimeupenda nahitaji kujifunza ufundi simu je mafunzo haya yapo
ReplyDelete