CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Friday, 17 July 2020

USHIRIKI WA VETA KATIKA MAONESHO YA 44 YA BIASHARA YA KIMATAIFA (SABASABA)


Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt. Pancras Bujulu katika picha ya pamoja na wafanyakazi na wanafunzi wa VETA katika nyuso za furaha baada ya VETA kuibuka mshindi wa tatu kwenye kundi la Taasisi za Elimu, Utafiti na Uendelezaji Ujuzi kwenye maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Mwl. Nyerere jijini Dar es Salaam tarehe 1 hadi 13 Julai, 2020.

Matukio katika picha ni Dkt. Pancras Bujulu, Mkurugenzi Mkuu wa VETA akipata maelezo kutoka kwa walimu na wanafunzi alipotembelea banda la VETA katika maonesho ya 44 ya  Biashara ya kimataifa (Sabasaba) yaliyofanyika katika Viwanja Vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere barabara ya kilwa Jijini Dar Es Salaam tarehe 1 hadi 13 Julai, 2020. 




Matukio katika picha ni Peter Maduki, Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, akipata maelezo kutoka kwa walimu na wanafunzi alipotembelea banda la VETA katika Maonesho ya Biashara 44 ya Kimataifa Dar es Salaam, (Sabasaba) yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es salaam tarehe 1 hadi 13 Julai, 2020.



VIONGOZI MBALIMBALI WALIOTEMBELEA BANDA LA VETA KATIKA MAONESHO YA 44 YA BIASHARA YA KIMATAIFA (SABASABA) YALIYOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE BARABARA YA KILWA JIJINI DAR ES SALAAM. 

Katibu wa Bunge Ndg.Stephen Kigaigai akipata maelezo kuhusu ubunifu wa pikipiki kutoka kwa  Saimon Njovu wa Chuo cha VETA Dodoma.

Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Yose Joseph Mlyambina akitembelea katika banda la VETA .
Mkuu wa Utawala Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kanali Julius Kadawi akipata maelezo katika banda la VETA kwenye maonesho ya Sabasaba.


WANANCHI MBALIMBALI WALIOFIKA KATIKA BANDA LA VETA NA KUPATA MAELEZO



Wananchi wakipata taarifa mbalimbali zinazohusu mafunzo ya Ufundi Stadi walipotembelea banda la VETA katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yaliyofanyika Katika Viwanja Vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Barabara ya Kilwa Jijini Dar Es Salaam.

No comments:

Post a Comment