Tarehe
30 Juni, 2020, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Joyce
Ndalichako, ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi
cha Wilaya ya Kasulu, kinachojengwa katika Halmashauri ya Mji Kasulu, mkoani
Kigoma.
Katika
ziara hiyo Prof. Ndalichako aliongozana na Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini Mh.
Daniel Nswanzugwako, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Simon Anange, Mwenyekiti
wa Bodi ya Elimu na Ufundi Stadi Ndg. Peter Maduki, Mkurugenzi Mkuu wa VETA
Dkt. Pancras Bujulu, Wajumbe wawili wa Bodi ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi
Dkt. Ethel Kasembe na Dkt.Michael Mawondo, pamoja na viongozi wengine wa Chama na Serikali ya
Wilaya ya Kasulu.
Ujenzi
wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Kasulu unatekelezwa na Halmashauri ya
Mji Kasulu na kusimamiwa na Mshauri Elekezi, Chuo cha Ufundi Arusha, kwa
gharama ya shilingi bilioni 2.19 chini ya Mradi wa Kukuza Elimu na Ujuzi kwa
kazi zenye tija (ESPJ).
Ujenzi
wa Chuo hicho unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba 2020.
No comments:
Post a Comment