Mkuu
wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Charles Makongoro Nyerere, leo, tarehe 8 Februari 2023
amekutana na Menejimenti ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA)
kuweka mkakati wa upanuzi wa chuo cha ufundi stadi cha Wilaya ya Simanjiro,
mkoani Manyara.
Akizungumza
katika kikao kilichofanyika ofisi za VETA Makao Makuu jijini Dodoma, Mhe.
Nyerere amesema upanuzi wa chuo hicho utawezesha wananchi wengi zaidi wilayani
Simanjiro kupata mafunzo ya ufundi stadi.
Kikao
hicho pia kiliwahusisha Mwenyekiti wa
Shirika la ECLAT Development Foundation la Mkoani Manyara, Ndg. Peter Toima
Kiroya na Mwenyekiti wa Shirika la Upendo la Ujerumani Dkt. Dkt. Fred Heimbach,
ambao ambao mashirika yao ndiyo yaliyoanzisha chuo Chuo Cha Ufundi Stadi cha
Wilaya ya Simanjiro, kisha kukabidhi majengo ya chuo hicho kwa VETA mwaka 2019.
Mkurugenzi
Mkuu wa VETA, CPA. Anthony Kasore, amesema VETA imedhamiria kwa dhati kufanya
upanuzi wa chuo hicho ili kifikie viwango vilivyoweka vya vyuo vya ufundi stadi
vya Wilaya ili kutoa ujuzi stahiki kwa wananchi wa Wilaya hiyo.
Amesema
kazi ya upanuzi wa chuo hicho umeanza ambapo ujenzi wa bweni la wasichana,
nyumba mbili za walimu pamoja na karakana mbili za mafunzo unaendelea chuoni
hapo na umefikia asilimia 80.
CPA.
Kasore amesema tayari Mamlaka imeshatoa fedha kiasi cha Shilingi za
Kitanzania milioni 190 kwa ajili ya
kukamilisha ujenzi wa bweni la wasichana, nyumba ya walimu pamoja na karakana
za ufundi umeme na ufundi bomba unaotarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Mei,
2023.
Chuo
cha VETA Simanjiro kilianza kutoa mafunzo mwaka 2019 ambapo hadi sasa kimeweza
kudahili wanafunzi 82 katika fani za Uashi, Useremala pamoja na Uuungaji na
Uchomeleaji Vyuma.
No comments:
Post a Comment