Wakazi wa mkoa wa Katavi wametakiwa kuwasomesha vijana wao katika chuo cha ufundi stadi VETA Mpanda ili mkoa upate wataalamu watakaochochea shughuli za Kimaendeleo na kiuchumi katika mkoa huo. Maoni hayo yametolewa na Frank Atanas pamoja na Jesca Wambali ambao ni baadhi ya wakazi wa Mpanda ambapo wameiasa jamii kuondokana na mtazamo hasi wa kutodhamini na kuamini kozi zitolewazo katika chuo cha ufundi stadi VETA Mpanda.
Joshua Matagane ni mkuu wa chuo cha ufundi stadi VETA Mpanda amesema Mwamko wa Wazazi kupeleka Vijana wao katika Chuo hicho bado ni Mdogo,amesema vijana wanaotoka mkoa wa Katavi ni 34 kati ya 122 wanaohitimu katika kozi mbalimbali zinazotolewa chuoni hapo hivyo kawaomba Wazazi na Wakazi wa Mpanda kuwa na mwamko wa kuwapeleka Vijana wao kupata Elimu ya mafunzo ya ufundi stadi VETA ili waweza kujiajiri na Kuongeza Wataalam Wengi wa fani Mbalimbali ndani ya Mkoa wa Katavi. (Chanzo )
No comments:
Post a Comment