Mamlaka ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya
Juu,Sayansi, Teknolojia, Habari, Ufundi Stadi na Utafiti (RAAWU)wametia saini
Mkataba wa Kuunda Mabaraza ya Wafanyakazi wa VETA.
Hafla ya utiaji saini
imefanyika leo tarehe 12 Desemba, 2023, katika Ofisi za VETA Makao Makuu jijini
Dodoma na kushuhudiwa na viongozi wa VETA na RAAWU.
Kusainiwa kwa Mkataba
huo wa miaka mitatu (2023 – 2026) kunatoa fursa ya kuanza kwa mchakato wa
kuunda mabaraza ya Wafanyakazi wa VETA kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu
za ushirikishwaji wa Wafanyakazi mahala pa kazi.
Katibu wa RAAWU
Taifa, Ndg. Joseph Sayo, amesema RAAWU itaendelea kushirikiana na uongozi wa
VETA katika kuhakikisha malengo ya VETA yanafikiwa na masuala yanayohusu
wafanyakazi yanashughulikiwa kwa wakati.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dkt. Prosper Mgaya, amesema VETA itatimiza wajibu wake katika kutekeleza Mkataba huo na kuushukuru uongozi wa RAAWU kwa ushirikiano wanaoendelea kuutoa kwa VETA.
Mkataba wa Kuunda
Mabaraza ya Wafanyakazi ulioisha muda wake ulidumu kwa miaka mitatu (2020 –
2023).
No comments:
Post a Comment