VETA Iringa ladies, leo
tarehe 20 Juni 2024, imenza michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa wa Timu za
Wanawake za Mpira wa Miguu katika hatua za makundi katika dimba la Jamhuri
Jijini Dodoma, huku ikiahidi kutwaa ushindi.
Timu hiyo ambayo imeapa
kutwaa kombe na kuiheshimisha VETA, leo imecheza na timu ya Tutes Academy ya
mkoani Songea, ambapo kwa taabu sana imekubali kupoteza mchezo huo kwa kufungwa
bao 1 kwa 0.
Akizumnguza baada ya
kumalizika kwa mchezo huo, kocha wa timu hiyo, mwalimu Laison Tuyembe, amesema
licha ya kupoteza katika mchezo wao wa kwanza wa leo, wanatazamia kufanya
vizuri zaidi katika michezo itakayofuata.
“leo tumepoteza kwa
kukubali kufungwa goli 1 kwa 0 na wenzetu kutoka mkoani Songea, lakini tuna
imani kubwa tutafanya vizuri katika mechi zilizobaki na kutinga hatua ya nusu
fainali na hatimae fainali na kutwaa ubingwa wa ligi hii” amesema kocha Laison
Kwa upande wake kapteni
wa timu hiyo, Jaqueline Laizer amesema anaimani watafanya vizuri katika michuano
hii kama walivyofanya huko Iringa na kuweza kuibuka Kidedea na kuwakilisha mkoa
wa Iringa katika ligi hii ya mabingwa wa mikoa wanawake ambayo imeanza kutimua
vumbi Jijini Dodoma.
“Ni kweli leo
tumepoteza katika mchezo wetu ila tunaamini tutafanya vizuri zaidi katika hatua
zinazofuata,” amesema.
Mkurugenzi wa timu ya VETA Iringa ladies,
Ramadhani Mahano ameshukuru uongozi wa chuo cha VETA Iringa kwa kufanikisha
timu hiyo kushiriki kikamilifu katika michuano hiyo tangu mkoani Iringa na
hatimaye kushinda na kuwa wawakilishi wa Mkoa wa Iringa katika ligi hiyo ya
mbingwa wa mikoa wanawake.
Ligi hiyo inadhaminiwa
na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Fountain Gate Academy ya
Jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment