CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Wednesday 26 June 2024

VETA Iringa Ladies yafa kiume

 

VETA Iringa ladies imeaga mashindano ya ligi ya mabingwa wa mikoa wanawake baada ya kukubali kufungwa mabao tatu kwa moja na timu ya Simba Queens ya mkoani Kilimanjaro, hapo jana tarehe 24 Juni 2024 katika viwanja vya Fontain Gate Academy, Jijini Dodoma.

VETA Iringa Ladies imeshia katika hatua ya makundi ikishika nafasi ya tatu katika kundi lililokuwa na timu tano huku ikishinda mechi mbili na kupoteza mechi mbili.

Akizumnguza kwa niaba ya timu, leo tarehe 25 Juni 204, mara baada ya kupita Makao Makuu ya VETA kwa ajili yakuaga na kutoa shukurani zao kutokana na ushirikiano walioupata kutoka kitengo  cha Uhusiano kwa Umma, kocha wa timu hiyo, mwalimu Laison Tuyebe  amesema japo wametolewa katika kinyang'anyiro hicho hawatakata tamaa kushiriki katika mashindano mengine.

“tumepita hapa leo kutoa shukurani zetu za dhati kwa ushirikiano mliotupa tangu tumeanza mashindano haya na sasa tujanarejea mkoani Iringa,” amesema kocha Laison

Kwa upande wake Mkurugenzi wa timu ya VETA  Iringa Ladies, Ramadhani Mahano amesema kutokusonga kwao mbele kumechagizwa na kukosekana kwa  wachezaji ambao wanaunda timu hiyo, wengi wakiwa ni wanafunzi wa mwaka wa tatu na mwaka wa pili ambao katika kipindi hiki cha ligi wao wapo  maeneo mbalimbali wakifanya mafunzo kwa vitendo hivyo wameshindwa kushiriki.

“Tumelazimika kuchukua wanafunzi wa mwaka wa kwanza kushiriki katika ligi hii kwani wanafunzi wa mwaka wa pili na mwaka wa tatu ambao ndio waozefu wapo maeneo mbalimbali wakijfunza kwa vitendo,” amesema  Ramadhani Mahano.

Timu ya VETA Iringa Ladies imerejea salama leo mkoani Iringa.

No comments:

Post a Comment