CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Saturday 29 June 2024

VETA KATIKA MAONESHO YA SABASABA 2024

Mhitimu wa fani ya mavazi na ubunifu wa nguo kutoka chuocha VETA Songea Riziki Ndumba akichukua vipimo vya nguo kwaajili ya kumshonea nguo  Esther Peter Mgale mkazi wa ubungo Jijini Dar es salaam baada ya kutembelea banda la VETA katika viwanja vya J.K. Nyerere  tarehe 29 Juni 2024.

Esther Mgale amejikuta akipigwa na butwaa baada ya kuona  Riziki mwenye ulemavu wa viungo ana uwezo mkubwa wa kushona nguo bila kuhitaji msaada wa mtu mwingine kuanzia hatua za upimaji wa vipimo vya nguo, kukata nguo kwa kutumia mkasi, kutunga uzi kwenye sindano na hatimaye kushona nguo iliyokamilika.

 “kwa kweli nimepatwa na mshangao kumuona kijana Riziki akiweza kushona nguo bila kuhitaji msaada wa mtu mwingine , kweli hii nimara yangu ya kwanza kuja kwenye maonesho haya, nawasihii wakazi wenzangu wa Dar es salaam wafike katika banda la VETA kuna vitu vizuri” amesema Esther

VETA wapo katika maonesho hayo tangu tarehe 28 Juni mpaka yatakapo fikia kilele chake tarehe 13 Julai 2024. 


No comments:

Post a Comment