Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore,
akizungumza na waandishi wa Habari leo Februari 21,2025 katika Chuo Cha VETA
Mkoani Singida kuelekea maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanziahwa Kwake mwaka
1995.
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Stadi (VETA) imetangaza rasmi maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa
kwake mwaka 1995.
Akizungumza na wanahabari leo,
tarehe 21 Februari 2025, katika Chuo cha VETA Singida, Mkurugenzi Mkuu wa VETA,
CPA Anthony Kasore, amesema maadhimisho hayo yataangazia mafanikio, changamoto,
na mustakabali wa elimu ya ufundi stadi nchini.
CPA Kasore amesema kuwa katika
kipindi hiki vyuo vya VETA vilivyoenea kwenye mikoa na wilaya nchini kote
vitatoa huduma ya ufundi bure ya ukarabati wa miundombinu ya Serikali kama
majengo ya hospitali, zahanati, shule, ofisi za umma pamoja na kwa watu
wasiojiweza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho na kuonesha mchango wa elimu na
mafunzo ya ufundi stadi kwenye jami.
No comments:
Post a Comment