CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Tuesday, 5 May 2026

Wakufunzi 25 VETA waenda Finland kujifunza teknolojia ya madini

Wakufunzi 25 wa vyuo vya VETA nchini wanatarajia kuondoka kwenda nchini Finland kujifunza ujuzi wa teknolojia zinazohitajika katika uchimbaji na ukuzaji mnyororo wa thamani wa madini, kupitia mradi wa Mafunzo ya Ufundi Stadi kuelekea Upatikanaji Endelevu wa Madini Muhimu nchini Tanzania (Vocational Pathway to sustainable Critical Raw Minerals in Tanzania) unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya. 

Akizungumza katika hafla fupi ya kuwaaga wakufunzi hao, katika ukumbi wa mikutano wa NACTVET, Mikocheni jijini Dar es salaam, leo tarehe 5 Mei, 2026, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, amewaasa kwenda kufanya juhudi na za kujifunza ujuzi na maarifa mapya.

“ili kukidhi mahitaji ya soko la ajira lazima tutafute walio bora. Kwa hiyo mnakwenda Filand kutafuta ujuzi na kuhakisha kile kinachofundishwa na VETA lazima kiwe kinakidhi mahitaji ya sekta ya madini vizuri,” amesema Profesa Mkenda.

Profesa mkenda ameipongeza VETA kwa kubuni mradi unaohusisha mafunzo kwa wakufunzi, pamoja na ununuzi wa vifaa na amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa maono yake ya kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya elimu na mafunzo.

Ametumia fursa hiyo pia kuiomba Chemba ya Madini kukaa na VETA na wadau ili kutambua ujuzi unaohitajika katika sekta ya madini nchini.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri, Mwenyekiti wa Bodi ya ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Profesa Sifuni Mchome amesema katika kipindi chake amehusika katika kujadili mikataba takribani 11 inayohusu madini, hivyo uhitaji wa watenda kazi wenye ujuzi kuhusu madini ni muhimu ili kutekeleza miradi ianayohusu sekta hiyo hapa nchini.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore amesema kuwa mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano wa VETA na wadau wa maendeleo wakiwemo GIZ, GTK, SNL na REDU kutoka Finland, ambao ndio waliofanikisha mpango wa wakufunzi 25 wa VETA Kwenda kupata mafunzo nchini Finland.

CPA Kasore ameushukuru Umoja wa ulaya(EU) kwa kuridhaia na kuona kwamba mradi huo unaweza kutekelezwa na VETA kupitia wakufunzi wake.

“Kupitia mradi huu tumelenga Kwenda kuwafundisha wanachi 400 ambao wanatoka katika mazingira ambayo shughuli za madini zinafanyika, pamoja na kuongeza ushiriki wa wanawake na makundi maalum,” Amesema Kasore

Kwaupande wake Neema Lyimo kwa niaba ya wakufunzi wanaokwenda Finland amesema “Tunaelekea Finland tukibeba moyo mmoja, dhamira moja, na lengo moja: kuleta maarifa na ujuzi wa hali ya juu ambao utaifanya Tanzania kuwa nchi ya kweli inayoweza kusimamia na kunufaika na hazina yake ya madini muhimu”.




No comments:

Post a Comment