Katibu Tawala wa Mkoa
wa Singida, Dkt Fatuma Mganga, ameipongeza Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Stadi (VETA) kwa kubuni teknolojia
na bidhaa zinazolenga kuongeza tija kwa wakulima na wafugaj nchini.
Dkt Mganga ametoa
pongezi hizo leo, tarehe 4 Agasti, 2026 alipotembelea banda la VETA kwenye
Maonesho ya Sikuku ya Wakulima Kitaifa
(Nanenane), katika viwanja vya Dkt John Malecela, Nzuguni, jijini Dodoma.
“tumeona jinsi VETA
wanavyojitahidi kutengeneza mashine mbalimbali ambazo zinarahisisha kazi kwa
wakulima na wafugaji katika maeneo yetu. Tumeona mashine
mbalimbali
zinazowafaa wakulima na wafugaji kama ile ya kuchanganyia chakula cha mifugo,
mashine kama hizi zinaweza kusaidia sana wananchi,” amesema Dkt. Mganga.
Dkt Fatuma ameongeza
utumiaji wa mashine rahisi kama
alizoziona VETA zitasaidia kuongeza tija na faida zaidi katika
uzalishaji.
“Niendelee
kuwapongeza ndugu zetu wa VETA, naomba waendelee kushirikiana na wahitaji ambao ndiyo soko, ili tuweze kuendelea
kusukuma etekeleazji wa Dira 2050
ninaamini kwa hizi teknolojia wametuonesha lengo la Dira tutalifikia hata kabla ya 2050 kwasababu wanachi wengi watawezeshwa kwa mitaji iliyopo na mitambo inayotengenezwa na wabunifu kutoka veta,” ameongeza.
Katika hatua nyingine
Dkt Mganga ameiomba VETA kushirikiana na ofisi za Mikoa, Wilaya na halmashauri
ili kuweza kukutanishwa na watumiaji wa bidhaa na ubunifu mbalimbali, kwani
wapo vijana kupitia vikundi wanapatiwa pesa kwa ajili ya kuendesha miradi
mbalimbali ambao wanahitaji vifaa na mashine kwa ajili ya kutekeleza miradi
hiyo.
VETA inashiriki
Maonesho ya Nanenane kwa lengo la kutangaza fursa za mafunzo ya ufundi stadi yanayogusa
sekta za kilimo na mifugo; ubunifu waa teknolojia zinazosaidia kuongeza tija
kwenye kilimo na ufugaji; ubunifu wa bidhaa zinazosaidia kupanua soko na
kuongeza mnyororo wa thamani kwenye mazao ya kilimo na mifugo sambamba na
kaulimbiu ya maonesho hayo, “Tambua Soko, Ongeza Tija kutekeleza Dira 2050.”

.jpeg)


VETA's recognition for its agricultural and livestock innovations demonstrates the important role that vocational institutions can play in Tanzania's economic development. Technologies such as feed-processing machines, agricultural-processing equipment and solar-powered irrigation systems can help reduce production costs, improve efficiency and create new business opportunities. When selecting an exterior material, durability and low maintenance are important considerations. Fiberglass siding can be a practical choice for projects that need a reliable and attractive finish.
ReplyDelete