Tuesday, 31 January 2023
Friday, 27 January 2023
Tuesday, 24 January 2023
Sunday, 22 January 2023
MAANDALIZI YA UJENZI WA VYUO 64 VYA UFUNDI STADI VYA WILAYA NCHINI
Wednesday, 18 January 2023
Tuesday, 17 January 2023
Sunday, 15 January 2023
Saturday, 14 January 2023
Friday, 13 January 2023
VETA YAJIPANGA KUFANYA MAKUBWA 2023
Mamlaka ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imejipanga vyema kuhakikisha watanzania wengi
zaidi wananufaika na mafunzo bora ya ufundi stadi yanatolewa kupitia vyuo vyake
nchini kote.
Akitoa salamu za
mwaka mpya kwa Watanzania jijini Dodoma tarehe 4 Januari, 2023, Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore, alisema kwa mwaka 2023 VETA
imedhamiria kuongeza fursa zaidi za mafunzo ya ufundi stadi kwa watanzania ili kuwawezesha kujipatia
ujuzi utakaowawezesha kushiriki kikamilifu kwenye shughuli mbalimbali za
uchumi.
CPA. Kasore ametaja
baadhi ya matarajio ya Mamlaka hiyo kuwa ni kuongeza udahili wa wanafunzi
kutoka 90,000 kwa mwaka 2022 hadi 118,000 kwa mwaka 2023 na kumalizia ujenzi wa
vyuo 25 vya ufundi stadi vya Wilaya pamoja na kuratibu ujenzi wa vyuo vipya 64 vya Wilaya na chuo cha Mkoa wa Songwe.
“Tumejipanga vyema
kuhakikisha kuwa ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi vya Wilaya 63 nchini na ujenzi
wa chuo cha ufundi stadi na huduma cha Mkoa wa Songwe unatekelezwa kwa ufanisi…
Tunashukuru Serikali imeshatenga shilingi bilioni 100 katika mwaka wa fedha
2022/2023 kwa ajili ya kuanza ujenzi huo,” alisema.
Akizungumza kuhusu
mafanikio yaliyopatikana mwaka 2022, CPA Kasore alitaja baadhi ya mafanikio
kuwa ni pamoja na kukamilisha kwa asilimia 97 ujenzi wa vyuo 25 vya Wilaya kwa
kutumia nguvu kazi ya ndani yaani “Force Account” na uratibu wa ujenzi wa vyuo
vinne vya Mikoa ya Simiyu, Njombe, Geita na Rukwa.
Katika kuhakikisha mafunzo ya ufundi stadi yanatolewa kwa ubora, CPA Kasore alisema katika mwaka 2022, jumla ya mitaala 48 ilihuishwa ili kuendana na mahitaji halisi ya soko la ajira na kuakisi mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
Aidha, CPA Kasore
alisema VETA imeendeleza ushirikiano na wadau mbalimbali ili kuwafikia
watanzania wengi zaidi wenye mahitaji ya mafunzo ya ufundi stadi na kukidhi
mahitaji ya makundi mbalimbali kwenye jamii.
Alitaja baadhi ya
wadau hao kuwa ni Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu
kupitia mradi wa Uwanagenzi ambapo jumla ya vijana 3900 walipatiwa mafunzo na
Shirika la Maendeleo ya Ujerumani (GIZ) kupitia mradi wa E4D kutoa mafunzo kwa
vijana 4200 nchini.Wanufaika wote hao walipatiwa mafunzo hayo bila malipo.
CPA Kasore alitoa
shukrani kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan kwa kuendelea kutoa kipaumbele kikubwa kwenye elimu na mafunzo ya ufundi
stadi ili kuhakikisha watanzania wanajipatia ujuzi utakaowawezesha kushiriki
kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi na kuwezesha vijana kujiajiri.
“Mhe. Rais amekuwa na
malengo makubwa sana katika kuhakikisha elimu ya ufundi stadi inaimarika na
kutolewa ndani ya nchi na tumeshuhudia mengi yakifanyika kwenye eneo la
kuboresha miundombinu inayotumika kutoa mafunzo ya ufundi stadi… Tunamshukuru
sana,” Amesema
Kwa mujibu wa CPA
Kasore, moja ya changamoto inayoikabili Mamlaka hiyo ni kushindwa kuhimili
idadi kubwa ya watanzania wanaoomba nafasi za kupata mafunzo ya ufundi stadi
kwenye vyuo vya VETA ambayo anaamini itatatulia kwa kiasi kikubwa na ujio wa vyuo
vya Wilaya na Mikoa, huku Mamlaka hiyo ikiendelea kubuni njia mbadala za utoaji
mafunzo kwa watanzania.
Thursday, 12 January 2023
Wednesday, 11 January 2023
Tuesday, 10 January 2023
Bodi ya VETA yapongezwa uboreshaji na upanuzi wa utoaji mafunzo ya ufundi stadi nchini
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Francis Michael, ameipongeza Bodi ya Nane
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa usimamizi thabiti wa elimu na mafunzo
ya ufundi stadi nchini.
Akizungumza wakati wa
hafla ya kuiaga Bodi hiyo jijini Dodoma tarehe 9 Januari, 2023, Dkt. Michael
amesema miongoni mwa mambo yaliyosimamiwa vyema na Bodi hiyo ni ujenzi wa vyuo
vya ufundi stadi vya wilaya ambao umetekelezwa na VETA kwa kutumia nguvukazi ya
ndani, pamoja na ubunifu wa programu za mafunzo kwa kuzingatia mahitaji ya soko
la ajira na mwenendo wa nchi kiuchumi.
“Itoshe kusema kwamba
usimamizi wenu ulikuwa mzuri na mmeitendea vyema mipango mbalimbali ya VETA, hasa
Mpango Mkakati wa Tano (VCP V) wa mwaka 2018/2019 hadi 2022/2023 ambao ndo hasa
ulikuwa katika kipindi chetu cha usimamizi wa VETA… hongereni sana. ,” amesema.
Amesema Serikali ya
Awamu ya Sita imeipa kipaumbele kikubwa sana elimu na mafunzo ya ufundi stadi
na kwamba uendeshaji na usimamizi wake unapaswa kuwa imara na madhubuti.
Awali, Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA. Anthony Kasore, amesema katika kipindi cha
kuanzia mwezi Februari, 2020, VETA imepata mafanikio mbalimbali ikiwemo
uandaaji wa mitaala 54 kuendana na mahitaji ya soko la ajira, uanzishwaji wa
vyuo vipya 19 pamoja na utanuzi wa miundombinu 31 kwenye vyuo vya VETA nchini
na kuongeza udahili wa wanafunzi kwenye vyuo vya VETA kutoka 56,000 mwaka 2020
hadi 141,854 mwaka 2023.
Mwenyekiti wa Bodi ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Ndugu Peter Maduki, ameishukuru Serikali kwa
kuiamini Bodi hiyo na kuipa ushirikiano mkubwa katika kutekeleza majukumu yake
na hatimaye kuiwezesha VETA kupiga hatua katika utoaji wa mafunzo ya ufundi
stadi.
Monday, 9 January 2023
Sunday, 8 January 2023
Friday, 6 January 2023
Thursday, 5 January 2023
Wednesday, 4 January 2023
JIONEE UTEKELEZAJI WA MRADI WA UJENZI WA CHUO CHA UFUNDI STADI CHA WILAYA YA IKUNGI MKOANI SINGIDA
Fuatilia vipindi zaidi vya Ujuzi ni Maisha kupitia chaneli ya Youtube ya VETA VETA TANZANIA
Tuesday, 3 January 2023
KOZI YA HUDUMA ZA NYWELE NA TIBA YA UREMBO (HAIR DRESSING AND BEUTY THERAPY)
Fuatilia vipindi zaidi vya Ujuzi ni Maisha kupitia chaneli ya Youtube ya VETA VETA TANZANIA























.jpg)






