CONTACT US: VETA Head Office, P.O.Box 802 Dodoma Tanzania, Plot No. 18, Central business Park (CBP). E-mail: info@veta.go.tz / pr@veta.go.tz/ Telephone: +255 26 2963661 Mobile +255 755267489 Fax: +255 22 2863408 / Url: www.veta.go.tz

Sunday 19 November 2017

Jinsi ya Kujiunga na vyuo vinavyomilikiwa na VETA



VETA imeweka utaratibu maalum kwa ajili ya kujiunga ili kupata mafunzo katika vyuo inavyovimiliki. Utaratibu ni kama unavyoelezwa hapa chini:

VETA hutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi na katika mifumo mbalimbali;

 Kwa mafunzo ya muda mrefu, yyuo vyote hutangaza nafasi za kujiunga mwezi wa Agosti kila mwaka. Matangazo hutolewa katika vyombo vya habari nchini pamoja na kwenye tovuti ya www.veta.go.tz;

 Mwombaji ni lazima awe amemaliza elimu ya msingi, sekondari na kuendelea;
Mwombaji huchukua fomu katika chuo chochote kilichopo karibu.  Fomu hizo zina taarifa ya vyuo vyote vinavyomilikiwa na VETA, ikiwa ni pamoja na fani zinazofundishwa na mahali chuo kilipo na kama ni kutwa au bweni;

Mwombaji anaruhusiwa kufanya mtihani wa kujiunga mkoa aliochukua fomu lakini anaweza kuchagua kusoma mkoa wowote anaochagua kulingana na mahitaji yake; 
 Mwombaji anatakiwa kufanya mtihani wa kujiunga (Aptitude Tests) mwezi Oktoba na wale wanaofanikiwa kuchaguliwa hupewa taarifa mwezi Decemba ili kuanza masomo Januari mwaka unaofuata;

Mwombaji anayefanikiwa hupewa barua ya kujiunga inayofafanua mahitaji yote muhimu. Mahitaji yanatofautiana toka chuo kimoja hadi kingine na kutegemeana na fani aliyoomba, na pia kama ni kutwa au bweni;

Kwa utaratibu huu Mwombaji anaanza kujiunga na daraja la 1(Level 1) ambalo ni daraja la chini. Waombaji wanaoendelea madaraja ya juu (Level II-III) vigezo ni ufaulu wa daraja husika unamwezesha kupanda daraja lingine.
                             

29 comments:

  1. Hivi mwombaji anatakiwa aje na nini ili aweze kujiunga

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ratifa Mary Sina cheti chochote ninataka kujiunga kwenye chuo chenu

      Delete
  2. Kunauwezekano wa kuwanza na short cource,na mwaka wa masomo wa long cource kuendelea nayo

    ReplyDelete
  3. Nataka kujua mwaka huu 2018 matokeo ya Veta songea yanapatikana kwenye link gani?.

    ReplyDelete
  4. Nataka kujua gharama za kozi ya ushonaji veta kihonda morogoro asante
    Na pia kama naweza kupata mawasiliano

    ReplyDelete
  5. Nataka kujua gharama za kozi ya ushonaji veta kihonda morogoro asante
    Na pia kama naweza kupata mawasiliano

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hi naomba nipate mawasiliono yenu Nina mtoto

      Delete
  6. mtoto wangu ana four ya 32 atapata kozi gani

    ReplyDelete
  7. Nikitaka kujiunga niwe na vigezo gani

    ReplyDelete
  8. Nahitaji short course ya ususi na urembo kwa ajili ya mke wangu. Je, ipo? Na utaratibu ukoje!

    ReplyDelete
  9. Je, course ya driving hutolewa kwa muda gani? Na gharama zake zikoje? Na ni sifa gani anatakiwa kuwa Nazo mwombaji?

    ReplyDelete
  10. Fomu lazima zichukuliwe shulen au??

    ReplyDelete
  11. Nataka kujua gharama za kujifunza ushonaji

    ReplyDelete
  12. Nahtaji kujua gharama za ususi na urembo short courts kwa chuo cha mlndzi gharama ya Ada shilingi ngapi

    ReplyDelete
  13. Nahitaj kujiunga veta kusomea ppf gharama yake inakuwaje

    ReplyDelete
  14. nataka kujua 2019-2020 bdo fom hazijatoka?

    ReplyDelete
  15. nataka kujua 2019-2020 bdo fom hazijatoka?

    ReplyDelete
  16. Kama Nimesoma short course naweza kujiunga na level ngapi

    ReplyDelete
  17. Semina za mafundi walio pata elim mitaan itafanyika mwezi gani

    ReplyDelete
  18. Nahitaji kujua mawasilino ya chuo cha veta shinyanga

    ReplyDelete
  19. Nataka kujiunga beta,Ni sifa zioi zinaitajika??

    ReplyDelete
  20. Nina umri wa miaka 37,elimu std 7,naitaji kujiunga na elimu ufundi wa magari,VP ntapokelewa?Jackson mkongwe arusha

    ReplyDelete
  21. ICT level III inapatikana chuo gani ukitoa chuo cha veta kipawa

    ReplyDelete
  22. naomba kuuliza form znatoka lin za yuo

    ReplyDelete
  23. nahitaji fomu ya kjiunga na level III ya chuo cha veta dar es salaam naipataje

    ReplyDelete