Chuo cha ufundi stadi VETA Mkoani
Shinyanga, kimezindua mafunzo mapya ya ufundi wa Mitambo Mikubwa (Heavy Duty Equipment
Mechanics), mafunzo ambayo yatasaidia vijana wengi kupata ajira kwa urahisi
ndani ya Migodi na katika shughuli za ujenzi wa barabara.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa
kozi hiyo tarehe 19 Februari 2018 kwenye chuo cha VETA Shinyanga, Kaimu Mkurugenzi wa Soko la Ajira, Mipango na
Maendeleo wa VETA, Hildegardis Bitegera alisema kuwa kozi hiyo imeanzishwa baada ya utafiti wa soko la ajira kubaini
uhitaji mkubwa wa mafunzo ya ufundi stadi kwa ajili ya kusaidia sekta ya madini
katika mikoa ya kanda ya ziwa.
Alisema, katika
hatua ya awali baada ya utafiti VETA
Shinyanga ilianzisha kozi ya Ukataji na Ung’arishaji vito (Gemstone cutting
Carving and Polishing) na kufatiwa na kozi ya Uendeshaji wa Mitambo Mikubwa
(Plant Operations) na hatimaye kozi ya Ufundi wa Mitambo Mikubwa kwa ufadhili
wa Serikali ya Canada chini ya Shirika la CICan kupitia mradi wa Uimarishaji
Mafunzo kwa ajili ya Ajira (ISTEP).
“Leo tunawaambia watu, hasa vijana
kuwa tuna kozi mpya yenye fursa kubwa ya ajira na kwa hivyo waje wajifunze. Kwa
upande mwingine, tunawaambia waajiri, hasa katika upande wa shughuli za uziduzi
(extractive) na ujenzi kuwa watarajie kutoka kwetu nguvukazi yenye ujuzi na
mahiri kwenye ufundi wa mitambo mikubwa,” alisema.
Aliongeza kuwa, VETA inatarajia vilevile kuongeza kozi
za Uchimbaji, Ulipuaji,na nyingine zinazohusiana na sekta ya madini.
Naye Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga Afridon Mkhomoi,
alisema kuwa uanzishwaji wa kozi hiyo umewezekana kwa ushirikiano mzuri wa vyuo
marafiki katika utekelezaji wa mradi wa ISTEP ambavyo ni Chuo cha New Caledonia
na Chuo cha the Rockies vya nchini Canada.
Alisema, pamoja na mafunzo mengine
ya uwezeshaji kwa Menejimenti, Walimu na Wafanyakazi wengine, vyuo marafiki
walitoa mitambo na vifaa vingine vya kufundishia kwa ajili ya kozi hiyo.
Aliishukuru Serikali ya Canada na
chuo cha College of New Colidonia (CNC) kwa ufadhili walioutoa wa vifaa hivyo
vya kujifunzia kutengenezea mitambo ambavyo vimewezesha mafunzo kuanza mara
moja.
Alisema, msaada huo ulichangia
katika kuanzisha kozi kwa kudahili wanafunzi 20, ambao kati yao 16 ni wa kiume na wanne ni wa
kike.
“Natoa wito kwa vijana mkoani
Shinyanga kuichangamkia kozi hii mpya ambayo itawapatia ajira kwa urahisi ndani
ya migodi kwa kutengeneza mitambo ambayo itakuwa ikiharibika sababu wataalamu
wake ni wachache,” alisema.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Mhandisi Thomas Katebalirwe, matarajio ya Serikali ni kupata watalamu wengi wa
ufundi wa mitambo hapa nchini.
Aliwaomba VETA kuendesha kwa ufanisi
mkubwa kozi hiyo akiamini kuwa baada ya miaka michache chuo cha VETA Shinyanga
kitakuwa chuo cha mfano kwa mafunzo yanayohusiana na shughuli za uchimbaji na
uchakataji madini.
Aidha mwakilishi kutoka Chuo cha New Colidonia (CNC), Romana
Pasca, alisema wameamua kufadhili vifaa kwa ajili ya mafunzo ili Tanzania ipate
kuongeza idadi kubwa ya wataalamu wa kutengeneza mitambo kutoka ndani ya nchi,
pamoja na kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.
Nao baadhi ya wanafunzi wanaosoma
mafunzo hayo mapya akiwamo Calvin Msafiri, waliipongeza Serikali kwa
kushirikiana na nchi ya Canada kuanzisha kozi hiyo mpya ambayo wana matumaini
kuwa itawapatia ajira kwa urahisi na kuinua uchumi wa maisha yao.
Mkuu
wa chuo cha VETA mkoani Shinyanga Afridoni Mkhomoi akisoma taarifa ya chuo
hicho juu ya Kozi mpya ya Ufundi wa
Mitambo Mikubwa.
Kaimu
Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Thomas Katebalirwe,
akizungumza kwenye uzinduzi wa kozi mpya ya Ufundi wa Mitambo Mikubwa (Heavy
Duty Equipment Mechanics) na kusema kuwa serikali inatarajia matokeo makubwa ya
kupata wataalamu wake wengi wa ndani ya nchi wa kutengeneza mitambo hiyo
mikubwa.
Mwakilishi
wa Chuo cha New Colidonia Romana Pasca, akizungumza kwenye uzinduzi wa kozi mpya
ya Ufundi wa Mitambo Mikubwa (Heavy Duty Equipment Mechanics). Kushoto kwake ni
mwakilishi mwenzake kutoka chuo hichohicho, Craig Hull.
Baadhi
ya vifaa ambavyo vijana watakuwa wakijifunzia kutengeneza mitambo mikubwa
katika mafunzo hayo mapya.
Mm naitwa samwel msuya niko dar es salaam nilikuwa naomba kuuliza kozi kwa kipindi hichi zinaanza lini za planting oparetor tafadhali naomba mawasiliano ya simu ya mkononi zangu ni 0679202500
ReplyDeleteSawa ada shingapi
ReplyDeleteNaitwa Edwin Philip nahitaji kujiunga na chuo nipo mwanza naweza jua Ada ya
ReplyDeleteNaitwa Edwin Philip nahitaji kujiunga na chuo nipo mwanza naweza jua Ada ya Sh ngapi na kukaa boding
ReplyDeleteHey mwenye namba za mawasioiano za chuoni naomba anisaidie maana nawish kujoin ila before nataka kuongea nao plz mwenye nazo
DeleteNiugeni mwana
DeleteNaitwa Monica makali nahitaji mafunzo ya excaveter je ada ni sh ngapi nania mda gani?
ReplyDeleteNaitwa Monica makali naitaji chuo cha mafumzo ya excaveter cha shinyanga je mafunzo yanaanza lini? Na ada sh ngapi? Na niyamda gani? Na ninaomba nisaidiwe contact no ya hapo chuoni mi niko Dodoma no yangu 0685510863
ReplyDeleteEnter your comment...nahitaji kujua kuhusu website yenu na cozi ya driving 2019 mwez wa 11 kama inapatikana namba yangu ni 0766021779
ReplyDeleteMwenye namba za mawasiliano chuoni shinyanga naombeni jaman
ReplyDeleteNahitaj kujua jinsi ya kujaza form zenu no 0765058930
ReplyDeletejamani mm naitwa kombo omary naombeni mnisaidie namba ya hapo chuoni namba yangu ni 0710062637
ReplyDeleteNaomba jaman njiunge namb yangu 0629579825
ReplyDeleteNamb yagu 0787866390
ReplyDeletemimi ni james kilingo nataka nijue ada ya ufundi mitambo shot cose na inakua kwa muda gan shot cose
ReplyDeletenasubili majibu yenu
ReplyDeleteNaitwa rehema maulidi naomba kujua Kam Kuna nafas ili niwez kujiunga na hii cozi nahitaj long course na ada ni Bei gani kwa kukaa boarding
ReplyDeleteKwa majina rehema maulidi naomba nafasi ya kusom hii coz mpya katika chuo chenu naomben Kam Kuna nafas naomb kujua pia ada kwa wale wa boarding namb ni 0747542351
ReplyDelete